KAMATI YA BUNGE YATEMBELEA UJENZI UWANJA WA NDEGE IBADAKULI SHINYANGA


Ujenzi wa Jengo la Abiria ukiendelea.
Na Marco Maduhu,SHINYANGA

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu,imetembelea kuona Maendeleo ya Ujenzi wa Uwanja wa Ndege uliopo Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga, na kutoa maagizo ujenzi huo ukamilike kwa wakati na ufanisi.

Ziara hiyo imefanyika leo Machi 14,2024.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo Seleman Kakoso, akizungumza kwenye ziara hiyo ya ukarabati na maboresho uwanja wa Ndege Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga, ameipongeza Serikali kwa matengenezo hayo, na kuagiza ukamilike kwa wakati na kwa ufanisi pamoja na kunufaisha wananchi.

“Tunaipongeza Serikali kwa ujenzi wa viwanja vya ndege, na ujenzi wa ukarabati wa uwanja huu wa ndege hapa Shinyanga msimamieni Mkandarasi akamilishe kwa wakati na kwa ufanisi, na mradi huu uache alama kwa wananchi kupitia CSR ikiwamo Ujenzi wa Shule, Zahanati au Kituo cha Afya,”amesema Kakoso.
Ameiagiza pia Wizara ya Ujenzi kwamba maeneo yote ya Viwanja vya Ndege yapimwe ili yawe na hatimiliki, pamoja na kuwekewa alama za mipaka ili wananchi wasije kuvamia maeneo hayo na kusababisha Mgogoro pamoja na kulipa fidia wananchi wasio stahili.

Waziri wa ujenzi Innocent Bashungwa, amesema ujenzi wa ukarabati na uboreshaji wa Uwanja huo wa Ndege upo nyuma wa muda asilimia 30, lakini asilimia 80 ya vifaa vya ujenzi vipo site na Mkandarasi atajenga usiku na mchana ili kuukamilisha kwa wakati.

Kaimu Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Dorothy Mtenga, amesema ujenzi wa ukarabati na maboresho wa Uwanja huo wa Ndege, amesema umeanza Rasmi Aprili 5 mwaka jana na unatarajiwa kukamilika Oktoba 4 mwaka huu kwa gharama ya Sh.bilioni 49.1 na ujenzi kwa sasa upo asilimia 10.4.

Amesema ujenzi huo wa Uwanja wa Ndege umetoa ajira 115 ambapo Wazawa wameajiriwa watu 100.
Ujenzi wa Jengo la Abiria ukiendelea.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments