NAIBU WAZIRI BYABATO: IMARISHENI UHUSIANO WA TANZANIA NA KENYA, MASHIRIKA YA KIMATAIFA


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki, Mhe. Stephen Byabato (Mb.) ametembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Kenya na kuzungumza na watumishi wa ubalozi wa Tanzania jijini Nairobi.

Pamoja na mambo mengine, Mhe. Byabato amewataka watumishi wa ubalozi huo kuendelea kuimarisha uhusiano kati ya Tanzania na Kenya pamoja na Mashirika ya Umoja wa Mataifa yaliyopo jijini Nairobi.

Katika hatua nyingine, Waziri Byabato amekutana na kupata chakula cha jioni na Wabunge wa Tanzania wanaoiwakilisha nchi katika Bunge la Afrika Mashariki.

Aidha, Mhe. Byabato alitumia fursa hiyo kuwaasa na kuwakumbusha Wabunge kuendelea kuiwakililisha vyema Tanzania na kusimamia maslahi na misimamo ya nchi yetu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post