BASI LA KEMEBOS SECONDARY LAPATA AJALI LIKIPELEKA WANAFUNZI GEITA


Na Mariam Kagenda _ Kagera

Basi la Shule ya Sekondari Kemebos lenye namba za usajili T 770 DSQ limepata ajali na kuua mwanafunzi mmoja na kujeruhi wengine sita katika Kata ya Kimwani Wilayani Muleba Mkoani Kagera   wakati likisafirisha wanafunzi kutoka Bukoba kuelekea Mkoani Geita.

Mkuu wa Wilaya ya Muleba Dkt. Abel Nyamahanga amesema kuwa ajari hiyo imetokea usiku wa kuamkia leo majira ya saa nane za usiku Kata ya Kimwani Wilayani Muleba ambalo lilikuwa na jumla ya wanafunzi 35.

Dkt. Nyamahanga amesema kuwa Mwanafunzi  huyo ni wa kidato cha tano aliyejulikana kwa jina la Frank Matage mwenye umri wa miaka 17 wa shule ya Sekondari Kemibos iliyoko manispaa ya Bukoba  huku majeruhi hao sita wote wamelazwa katika Hospital ya rufaa ya Mkoa Bukoba .


Aidha Dkt. Nyamanga amesema kuwa kwa taarifa za awali zinaeleza chanzo cha ajali hiyo ni Mwendo kasi wa Dereva ambaye alishindwa kukata kona.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments