Polisi wameanzisha uchunguzi kuhusu kilichotokea kuhusu mauaji ya mwanamke mwenye umri wa miaka 23 nchini Uganda.
Katika taarifa, msemaji wa polisi Fred Enanga aliripoti kuwa Chandiru Judith aliuawa na mumewe mwenye umri wa miaka 48, Agunda James.
Kulingana na polisi, mauaji hayo ya shambulizi yalitokea siku ya Ijumaa, Machi 1,2024 baada ya mzozo kuhusu Chandiru kumnyima Agunda haki ya ndoa.
"Polisi wa eneo katika Mkoa wa Nile Magharibi na Ayivu Mashariki CPS wanamshikilia Agunda James, jamaa mwenye umri wa miaka 48 wa seli ya Obaru, kata ya Ombokolo, kwa mauaji ya kumpiga mkewe, Chandiru Judith, mwenye umri wa miaka 23 usiku wa tarehe 1.03.2024, kwa kunyimwa haki za ndoa," alisema.
Uchunguzi wa awali ulibaini kuwa wanandoa hao hawakuwa wamefanya mapenzi kwa muda licha ya kulala kitanda kimoja.
Judith alikuwa amemshutumu mumewe kwa kutokuwa mwaminifu na siku alipokufa, Judith alitoka kitandani na kulala chini.
“Habari zilizokusanywa zinaonyesha kuwa wanandoa hao wamekuwa wakilala pamoja lakini bila ya kujamiiana, baada ya mwathiriwa kumtuhumu mumewe kuwa na mahusiano ya nje ya ndoa, usiku wa tarehe 1.03.2024 mtuhumiwa alizua ugomvi na mke na kuondoka zake kitanda chake na kulala kwenye godoro jingine," polisi walisema.
Akiwa amekasirishwa na kitendo chake, inasemekana Agunda alimshika Judith na kumpiga pembeni ya mbavu, na kumwacha katika maumivu makali. Baadaye alipoteza maisba yake kutokana na majeraha. Kisha akajisalimisha kwa polisi ambao waliandikisha tukio na kuanza uchunguzi mara moja.