NTOBI AJITOSA KUTETEA UENYEKITI CHADEMA MKOA WA SHINYANGA

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa Shinyanga,  Emmanuel Ntobi anatarajia kutetea nafasi yake ya Uenyekiti wa Chadema Mkoa Shinyanga kwenye uchaguzi wa CHADEMA ambao unatarajiwa kufanyika Machi 26, 2024.

Ntobi ambaye aliwahi kuwa Diwani wa Ngokolo, Manispaa ya Shinyanga na Mwenyekiti wa Madiwani Kanda ya Serengeti CHADEMA anasema amejipima, amejitathimini, ameona anatosha.

 Amesema kutokana na maombi mengi ya wanachama wa CHADEMA Mkoa wa Shinyanga amekubali kuendelea kuongoza Mkoa huo kwa miaka mingine mitano.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post