PAC YATEMBELEA MRADI WA MAJI TINDE - SHELUI


Mkurugenzi wa KASHWASA Mhandisi Patrick Nzamba akiionesha mchoro wa ujenzi wa mradi wa maji ya Ziwa Victoria, Kamati ya kudumu ya Bunge ya hesabu za serikali (PAC) mradi wa maji ya Ziwa Victoria Buchama -Tinde ambao pia utapeleka maji Shelui

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya hesabu za serikali Japhet Hasunga akizungumza baada ya kukagua mradi huo akiwa na wajumbe wa Kamati

Na Stella Homolwa, Shinyanga 

Kamati ya kudumu ya Bunge ya hesabu za serikali (PAC) imetembelea mradi wa tenki la maji ya Ziwa Victoria wa Buchama- Tinde ambao utapeleka maji Shelui, ili kuona utekelezaji wake na iwapo kama wananchi waliolengwa wamefikiwa ili kuona thamani halisi ya fedha zilizotolewa na serikali.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya PAC Japhet Hasunga akizungumza baada ya kufika kwenye mradi huo leo Machi 27, 2024, amesema watakaa na Katibu Mkuu Wizara ya maji ili kuona kama fedha Shilingi bilioni 24 zilizotengwa kutekeleza mradi kama zimefikia lengo lililokusudiwa.

Amesema mradi huo wa maji ambao unasimamiwa na Wizara ya maji ulikusudia kufikia vijiji 34 vikiwemo 22 kwa upande wa Shinyanga na 12 Shlui, ili kuwawezesha wananchi kupata huduma karibu na kumaliza changamoto ya maji.

“Sisi ukituambia mradi huu ilikuwa ni kusanifu na kujenga maana yake ni kwamba hakutakuwa na fedha za nyongeza, kazi yetu ni kuona fedha zilizotolewa Sh Bilioni 24 zimetumikaje katika mradi huu na kama vijiji vingine havina maji tutapata majibu kutoka Wizarani”, amesema Hasunga.

Awali akitoa taarifa ya mradi huo mhandisi Tito Alex kutoka Wizara ya Maji amesema mradi huo umekamilika kwa awamu ya kwanza na unatarajia kutoa huduma kwa watu zaidi ya laki moja ili kusogeza huduma karibu kwa wananchi.

Naye mjumbe wa Kamati hiyo Ravia Faina (Mbunge wa Makunduchi) Wilaya ya Kusini Unguja,amesema inasikitisha kuona Kijiji lilipojengwa tenki la maji wananchi wake hawana huduma ya maji na kubainisha kuwa jambo hilo litafikishwa kwenye Wizara.

Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Tinde Jafari Kanolo ameiomba Kamati hiyo kusaidia ili wananchi wa Kijiji cha Buchama wapate huduma ya maji safi na salama, kwa kuwa mradi huo umejengwa katika eneo hilo na wao ndiyo waangalizi wakuu wa Mradi.
Mkurugenzi wa KASHWASA Mhandisi Patrick Nzamba akitoa maelezo kwa Kamati ya kudumu ya Bunge ya hesabu za serikali (PAC) mradi wa maji ya Ziwa Victoria Buchama -Tinde ambao pia utapeleka maji Shelui
Mhandisi Tito Alex kutoka Wizara ya maji akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi wa maji ya Ziwa Victoria Buchambi-Tinde hadi Shelui.
Diwani wa Kata ya Tinde Jafari Kanolo akizungumzia mradi huo
Mkurugenzi wa Shuwasa Mhandisi Yusuph Katopola wa kwanza kulia akiwa na wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya hesabu za serikali baada ya kutembelea mradi wa maji ya Ziwa Victoria Buchama -Tinde.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya kudumu ya bunge ya PAC.
Ukaguzi wa Mradi unaendelea.
Wajumbe wakiwa eneo la Mradi.
Wajumbe wakiwa eneo la Mradi
Kazi inaendelea.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya hesabu za serikali Japhet Hasunga akizungumza baada ya kukagua mradi huo akiwa na wajumbe wa Kamati.
Mjumbe wa Kamati Geoffrey Mwambe akitoa ushauri baada ya kukagua Mradi.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments