TANZANIA NA RWANDA KUBORESHA USHIRIKIANO BANDARI YA DAR ES SALAAM


Na Mwandishi Wetu, RWANDA 

Tanzania na Rwanda kwa pamoja zimekubaliana kuweka mazingira bora yatakayosaidia kuongeza ufanisi wa matumizi ya Bandari ya Dar es salaam ikiwa ni moja ya njia za kusaidia kukuza uchumi wa nchi hizo mbili.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba (Mb.) wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Kigali, nchini Rwanda pamoja na waziri mwenza wa Mambo ya Nje wa Rwanda Mhe. Dkt. Vincent Biruta.

Rwanda imeongeza wigo wa matumizi ya Bandari ya Dar es salaam kwa zaidi ya asilimia 80 kwa usafirishaji wa mizigo yake.

Mbali na usafirishaji, Waziri Makamba na Waziri Biruta wamejadili masuala mengine ya kipaumbele kwa nchi hizi mbili kushirikiana ikiwemo Nishati, Kilimo na Teknolojia.
 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments