BALOZI KIBESSE ATETA NA  GAVANA WA KISUMU, PROF. NYONG'O


Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Mhe. Dr. Bernard Kibesse amefanya ziara katika Kaunti ya Kisumu ambapo amekutana na kufanya mazungumzo na Mhe. Prof. Peter Nyon’go, Gavana wa Kaunti ya Kisumu tarehe 8 Februari 2024.

Mhe. Balozi Kibese na Gavana Nyong’o wamekubaliana kuandaa mkutano wa ujirani mwema kati ya mikoa ya Tanzania na Kenya inayopakana kwenye eneo la Ziwa Victoria ili kuweka mikakati ya kuimarisha ushirikiano wa kijamii, kibishara na kiusalama katika maeneo hayo ikiwemo Mwanza na Mara kwa upande wa Tanzania na Kisumu na Migori kwa upande wa Kenya

Vilevile wamekubaliana kufuatilia mpango wa kuwa na miundombinu ya pamoja hususan barabara inayopita kwenye mwambao wa Ziwa Victoria upande wa Tanzania na Kenya.

Gavana Nyong'o amemzawadia Balozi Kibesse kitabu ambacho ameandika.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post