KAMATI YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI YATEMBELEA MGODI WA ALMASI MWADUI, YAIPONGEZA SERIKALI NA MGODI

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetembelea Mgodi wa Almasi Mwadui wilayani Kishapu mkoani Shinyanga kwa ajili ya kuona shughuli zinazofanywa na mgodi huo pamoja na kuona Bwawa Jipya la Majitope sambamba na Mradi wa Nyumba Mbadala zilizojengwa na Kampuni ya Williamson Diamonds Limited kwa ajili ya kaya zilizoathirika na tukio la kupasuka kwa bwawa la Tope Laini lililotokea Novemba 7,2022 kisha tope kwenda kwenye makazi ya watu na kuleta madhara mbalimbali.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo iliyofanyika leo Jumapili Februari 18,2024, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini, Mhe. Shaban Kirumbe Ng'enda amesema Kamati hiyo imewasikiliza wananchi wanaozunguka mgodi huo pamoja na viongozi wa Mgodi na kuchukua malalamiko madogo yaliyopo ambayo wanayapeleka serikalini ili yashughulikiwe.

"Katika ziara hii ya kamati tuliyoambatana pia na Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa, tumepata nafasi ya kuwasikiliza wananchi na tumepata nafasi ya kuwasikiliza watu wa mgodi, pamoja na mambo makubwa yaliyofanyika lakini yapo baadhi ya malalamiko madogo madogo ambayo tunaweza kukaa chini na kuyatatua kwa hiyo tunawaomba wananchi muwe watulivu sisi tunakwenda kukaa na serikali pamoja na mgodi tupitie haya mambo yote mliyoyalalamikia halafu tuone namna serikali itakuja kutatua hayo mnayoyalalamikia",amesema Ng'enda.

"Kuhusu hayo mnayoyaomba juu ya kuomba kuboreshewa zaidi ikiwemo kuletewa maji na umeme tunayakabidhi kwa serikali mkuu wa wilaya yuko hapa, yatafanyiwa kazi. Baada ya muda mtaona majibu kwa serikali hii inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni sikivu itakamilisha. Hongereni sana, endeleeni kuwa watulivu endeleeni na maisha",ameongeza Ng'enda.

Aidha kamati hiyo imeishukuru serikali na mgodi kwani baada ya baada ya tatizo la kupasuka kwa bwawa kutokea walichukua hatua kubwa ya kuhakikisha hakuna maisha ya mwananchi yanapotea.

"Tunaendelea kuwapa pole wananchi kutokana na kubomoka kwa bwawa hili, tunaupongeza sana mgodi pamoja na serikali kwa kuchukua hatua ili kuhakikisha wananchi wanapata haki zao.

Tumejionea nyumba mpya zilizojengwa ni bora kuliko zile za zamani walizokuwa wanaishi wananchi kabla janga la bwawa kubomoka", amesema.

Kwa upande wake, Kaimu Meneja wa Mgodi wa Almasi Mwadui Mhandisi Shaghembe Mipawa, ambaye ni Mhandisi Mkuu wa Mgodi huo, amesema tukio hilo la kubomoka bwawa la Mgodi wa Almasi Mwadui likitokea Novemba 7 Mwaka 2022, na kuathiri wananchi 286 katika kaya 50 wa vijiji vya Ng'wang'holo na Nyenze na wamelipwa fidia.

'Tumepokea maelekezo yaliyotolewa na Kamati ya bunge, tutayafanyia kazi",ameongeza.

Amesema baada ya tukio hilo, walikuwa pamoja na wananchi kwa kuwapatia huduma zote za kijamii ikiwemo chakula, maji, makazi na malazi pamoja na kupeleka  watoto shule.

Afisa Mahusiano Mgodi wa Almasi Mwadui Bernard Mihayo, amesema nyumba za fidia ambazo zilipaswa kujengwa ni 48 na 42 zimekamilika na wananchi wameanza kuishi, mbili ujenzi wake unaendelea,ambapo nyumba nne wananchi waligoma kujengewa walipwe fidia ya pesa hivyo watalipwa.

Diwani wa Mwadui Luhumbo Francis Manyanda, akijibu swali aliloulizwa na Kamati hiyo juu ya wananchi kushirikishwa ulipwaji fidia, amesema kwamba jambo hilo lilikuwa na uwazi na wananchi wote wameshirikishwa hadi hatua ya mwisho.

Nao baadhi ya wananchi walioathirika na kubomoka kwa bwawa la maji tope akiwemo Suzana Ngasa Japa na Samwel Seni wameishukuru Kampuni ya Williamson Diamonds Limited na serikali kwa kuwajengea nyumba na kuwapa fidia mbalimbali huku wakiomba serikali kuwaboreshea zaidi mazingira ikiwemo kuwasogezea huduma za maji na umeme.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Kaimu Mwenyekiti wa Kamati kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Shabani Ngenda akizungumza wakati wa ziara hiyo. Picha na Kadama Malunde _Malunde 1 blog
Kaimu Mwenyekiti wa Kamati kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Shabani Ngenda akizungumza wakati wa ziara hiyo
Kaimu Meneja wa Mgodi wa Almasi Mwadui Mhandisi Shaghembe Mipawa, ambaye ni Mhandisi Mkuu wa Mgodi huo akiwaonesha wajumbe Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Shimo la kuchimba Madini ya Almasi.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakiwa kwenye Shimo la kuchimba Madini ya Almasi.
Muonekano wa sehemu ya Shimo la kuchimba Madini ya Almasi.
Mhandisi Mkuu wa Mgodi wa Almasi Mwadui Shaghembe Mipawa akitoa maelezo kwenye ziara hiyo ya Kamati ya Kudumu ya Bunge Nishati na Madini.
Mhandisi Mkuu wa Mgodi wa Almasi Mwadui Shaghembe Mipawa akitoa maelezo kwenye ziara hiyo ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini.

Muonekano wa sehemu ya bwawa Jipya la kuhifadhia Majitope
Mhandisi Mkuu wa Mgodi wa Almasi Mwadui Shaghembe Mipawa akielezea namna walivyojenga bwawa Jipya la kuhifadhia Majitope na kuanza uzalishaji wa Madini ya Almasi,mara baada ya bwawa la awali kupasuka.

Mhandisi Mwelekezi wa Mradi wa Ujenzi wa bwawa la tope katika mgodi wa Williamson Diamond Limited, Mhandisi Anael Macha ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kizalendo inayomilikiwa Watanzania ya City Engineering akielezea uimara wa bwawa jipya la tope laini katika Mgodi wa Williamson Diamond Limited.
Mhandisi Mwelekezi wa Mradi wa Ujenzi wa bwawa la tope katika mgodi wa Williamson Diamond Limited, Mhandisi Anael Macha ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kizalendo inayomilikiwa Watanzania ya City Engineering akielezea uimara wa bwawa jipya la tope laini katika Mgodi wa Williamson Diamond Limited.
Mhandisi Mkuu wa Mgodi wa Almasi Mwadui Shaghembe Mipawa akitoa maelezo kwenye ziara hiyo ya Kamati ya Kudumu ya Bunge Nishati na Madini.
Mhandisi Mkuu wa Mgodi wa Almasi Mwadui Shaghembe Mipawa akitoa maelezo kwenye ziara hiyo ya Kamati ya Kudumu ya Bunge Nishati na Madini.
Mwananchi akielezea namna walivyolipwa Fidia za Nyumba.

Afisa Mahusiano Mgodi wa Almasi Mwadui Benard Mihayo akitoa maelezo kwenye ziara hiyo ya Kamati ya Kudumu ya Bunge Nishati na Madini.

Muonekano wa sehemu nyumba zilizojengwa na Kampuni ya Williamson Diamonds Limited kwa ajili ya kaya zilizoathirika na tukio la kupasuka kwa bwawa la Tope Laini

Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa akizungumza wakati wa ziara hiyo

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments