UVCCM DODOMA YAWAANDAA VIJANA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA

 

Na Dotto Kwilasa,Dodoma


KATIBU wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya
ya Dodoma Mjini Isack Ngongi amewataka vijana kuungana kuhakikisha
chama kinashinda kwa kishindo katika uchaguzi wa serikali za mitaa na
uchaguzi mkuu.

Ngongi ameyasema hayo jijini hapa jana wakati akigawa vyeti wa wanafunzi
wa Chuo ya Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) na Chuo cha Madini
waliohitimu mafunzo ya itifaki, usimamizi wa mikutano na uongozi.

Amesema hivi karibuni kutakuwa na uchaguzi wa serikali za mitaa vijana
tumejipanga na hatutakubali kupoteza mtaa hata mmoja.

“Kuna chaguzi ziko mbele yetu sisi kama vijana tunatakiwa kuungana kuwa
kitu kimoja kuhakikisha CCM inashinda kwa kishindo. Tutahakikisha
tunatafuta kura nyumba kwa nyumba ili kuendelea kushika dola ambapo
ndio ndoto ya chama chochote cha siasa,”amesema

Kuhusu vijana waliohitimu mafunzo hayo Ngogi amewasisitiza kuwa na
heshima na kuwa mstari wa mbele kueleza mambo mazuri yanayofanywa
na serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dk.Samia.

Adhia amewahamasha vijana kuchukua fomu za kugombea nafasi
mbalimbali za uongozi katika uchaguzi ujao.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa UVCCM Tawi la Chuo cha Mipango na
Mujumbe wa Balaza la UVCCM Mkoa wa Dodoma Sebastiani Tarimo
alisema wanafunzi 65 wamehitimu mafunzo hayo na kupewa vyeti.

Amesema mafunzo hayo yalifanyika kwa siku mbili ambapo vijana hao
walishiriki na sasa wapo tayari kutumika katika shughuli mbalimbali za
chama na serikali.

Naye Muhitimu wa Mafunzo hayo ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya
Afya na Mazingira (MISO) Amina Paschal amesema mafunzo hayo yalikuwa
mazuri na yatasaidia katika kuongeza heshima na kupanua wigo wa
kutumikia chama katika shughuli mbalimbali.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post