DKT. EMMANUEL NCHIMBI KATIBU MKUU WA CCM


Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Katibu Mkuu mpya wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Emmanuel John Nchimbi mara baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo kwenye Kikao Maalum cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kilichokutana tarehe 15 Januari, 2024 Mjini Unguja Zanzibar.

***

Dkt. Emmanuel Nchimbi ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) akichukua nafasi ya Daniel Chongolo aliyejiuzulu.


Uteuzi wa aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Misri, Dk Emmanuel Nchimbi kuwa Katibu Mkuu wake mpya umefanyika leo Jumatatu Januari 15, 2024 wakati wa kikao cha Kamati Kuu ya CCM kisha kuthibitishwa na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) iliyofanyika mjini Unguja, Zanzibar

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post