MWENYEKITI SMAUJATA TANGA AHIMIZA UMUHIMU WA VITEGA UCHUMI KILA WILAYA


Mwenyekiti wa Smaujata Mkoa wa Tanga Hamis Ngota akizungumza wakati wa mkutano wake na wajumbe wa umoja huo uliofanyika Jijini Tanga
Oscar Assenga,TANGA

Mwenyekiti wa Smaujata Mkoa wa Tanga Hamis Ngota amehimiza umuhimu wa ushirikiano utakaokwenda sambamba na uanzishwaji wa vitega uchumi kila wilaya ambavyo vitakuwa ni chachu ya kuweza kuikwamua Jumuiya hiyo.


Mbota aliyasema hayo wakati wa mkutano wake na wajumbe wanaounda Jumuiya hiyo uliofanyika Jijini Tanga ambapo alisema hatua hiyo ni utekelezaji kwa vitendo maono ya viongozi wao wa Taifa.

Alisema viongozi wao umoja huo Taifa wameelekeza lazima kila mkoa uweze kuwa na kitega uchumi chake ambapo tayari kwa mkoa huo wameanza mchakato wa kufanikisha suala hilo.

“Viongozi wa Sumaujata Mkoa wa Tanga tujiathimini na tuhakikishe tunaunga mkono kauli mbiu ya Mwenyekiti wetu Taifa kwamba kila shujaa awe na kadi ya bima ya afya na kitega uchumi chake“Alisema

Aidha alisema kuwa wanataka kuwa na mradi katika mkoa ambao utasimamiwa na wilaya ambao utasimama ili kuweza kuwa rahisi kutekeleza miradi yao.

“Lakini kikubwa naombeni ndugu zangu mnipe ushirikiano kwa maana tuna mipango mingi mizuri ya kuukwamua umoja wetu huu kwa mkoa wa Tanga na tayati tuna mpango kazi ambao utawasaidia wanataka kwenda wapi na wanataka kufanya nini”Alisema Mwenyekiti huyo.

Hata hivyo aliwaomba ushirikiana ikiwemo kuhakikisha wanajitoa kwa nguvu zao kuhakikisha wanapata mafanikio makubwa kwani miradi itakapoanza kunahitajika usimamizi
 mzuri.

Akizungumzia suala kampeni ya kupinga ukatili wa Kijisnia na kusajili mashujaa Wazalendo ,Mwenyekiti huyo alisema kampeni hiyo ina umuhimu mkubwaa kwa jamii kutokana na kwamba elimu ambayo watakayokuwa wakiipata itawasaidia na kuwawezesha kupata uelewa wa namna ya kuepukana na hali hiyo.

"Kampeni hii ya kupinga ukatili wa kijinsia ni muhimu kwa jamii ya watanzania na sisi kupitia umoja wetu wa Smautaja tutahakikisha tunashiriki kikamilifu kwa kutoa elimu ambayo tunaamini itakuwa chachu ya kuweza kuondokana na vitendo hivyo kwenye jamii"Alisema 

Hata hivyo aliwaomba viongozi wa dini na jamii kwa ujumla kuona umuhimu wa kukemea vitendo hivyo ili viweze kuondoka kwani Tanzania inawezekana bila kuwa na vitendo hivyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post