MANYARA WASHEREKEA KUMBUKIZI YA KUZALIWA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN


 Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Cuthbert Sendiga ameongoza zoezi la upandaji wa miti lililoendana na ukataji wa keki kwa ajili kusherekea miaka 64 ya kuzaliwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. 

Akiongoza zoezi hilo la upandaji na kukata keki lililofanyika Januari 27, 2024 katika Shule ya Sekondari ya Katesh - Hanang, Mhe. Sendiga amesema Miti zaidi ya 3,000 imepandwa katika maeneo yaliyoathiriwa na maporomoko ya tope, mawe na magogo ikiwa ni njia mojawapo ya kurejesha uoto wa asili uliopotea kufuatia uharibifu mkubwa wa mazingira uliosababishwa na mafuriko yaliyotokea mwishoni mwaka mwaka jana.

Zoezi hilo lilihudhuriwa na Viongozi mbali mbali wakiwemo Waziri Mkuu mstaafu Fredrick Sumaye, Wakuu wa Wilaya wote wa Mkoa wa Manyara, wananchi pamoja na watoto walioadhirika katika maporomoko hayo.

Mkoa wa Manyara umejipanga kupanda miti milioni 10 kwa mwaka 2024.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post