MADHIMISHO WIKI YA SHERIA YAZINDULIWA SHINYANGA


 
Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme, amezindua Rasmi Maadhimisho ya wiki ya Sheria Nchini mkoani humo, na kutoa wito kwa wananchi wajitokeze kwa wingi kupata elimu ya kisheria na kutatuliwa matatizo yao kwa mujibu wa sheria.
Wiki ya sheria nchini ilianza kuadhimishwa Januari 24 mwaka huu, na itahitimishwa tarehe 30 na kufungwa Rasmi Februari Mosi, ambapo kwa Shinyanga yatafungwa katika Viwanja vya Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga.

Mndeme akizungumza kwenye uzinduzi huo leo Januari 27, 2024 ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Shinyanga, wajitokeze kwa wingi kwenye maadhimisho hayo ya wiki ya sheria, ili wapate elimu ya kisheria na kutatua matatizo yao kwa mujibu wa sheria na kudumisha Amani.
“Natoa wito kwa wananchi wote wa Mkoa wa Shinyanga kushiriki kwenye shughuli zote za utoaji wa elimu, kwa sababu wiki ya sheria imewekwa mahususi kwa ajili yenu, na wananchi wenye changamoto mbalimbali zinazohusu masuala ya kimahakama mfike katika eneo hili na kukutana na wataalamu wa sheria ili kupata ufumbuzi wa changamoto zinazowakabili,”amesema Mndeme.

“Nazitaka pia Taasisi zote zinazohusiana na masuala ya utoaji wa haki, kufanya kazi kwa kufuata kanuni na taratibu za nchi yetu na weledi wa Taaluma zenu, binafsi hua sifurahishwi hata kidogo na Malalamiko ya Wananchi kuhusu kutotendewa haki na baadhi ya vyombo ambavyo vimeaminiwa kutoa haki, tendeni haki,”amesema Mndeme.

Aidha, ametoa Rai pia kwa wadau wote wa haki jinai kuizingatia Kauli ya wiki ya maadhimisho ya sheria nchini ya mwaka huu 2024 kwa kufanya kazi ya kutoa haki, pamoja na mfumo mzuri unaosomana ili kurahisisha upatikanaji wa haki kwa wananchi.

“Kama Kauli Mbiu inavyosema kunahitaji kuwa na mfumo Jumuishi baina ya Taasisi zote za haki jinai, ambazo ni Jeshi la Polisi, Ofisi ya Taifa ya Mashitaka, Chama Cha Mawakili wa kujitegemea, Uhamiaji, Magereza, Takukuru, Mfumo huu ukisomana vizuri utasaidia upatikanaji wa haki kwa wakati,” ameongeza Mndeme.
Naye Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye ulemavu, ameviomba vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na Mahakama kuendelea kutenda haki kwa wananchi, na kwamba bila haki amani haiwezi kupatikana.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga Frank Mahimbali, amesema wiki hiyo ya Sheria nchini ni muda ambao Mahakama inaongea na wananchi kwa kutoa elimu juu ya masuala ya kisheria, na kutoa wito kwao waitumie kupata elimu hiyo.
Kauli Mbiu ya Maadhimisho ya wiki ya Sheria nchini mwaka huu 2024 inasema” Umuhimu wa dhana ya haki kwa Ustawi wa Taifa, nafasi ya Mahakama na wadau katika kuboresha mfumo wa haki jinai.”

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akizungumza kwenye uzinduzi wa Maadhimisho ya wiki ya Sheria nchini mkoani Shinyanga.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga Frank Mahimbali akizungumza kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya Sheria nchini mkoani Shinyanga.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye ulemavu akizungumza kwenye uzinduzi wa maadhimisho hayo ya wiki ya sheria mkoani Shinyanga.
Viongozi wakiwa meza kuu kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya sheria nchini mkoani Shinyanga.
Uzinduzi Maadhimisho ya sheria nchini mkoani Shinyanga yakiendelea.
Uzinduzi Maadhimisho ya sheria nchini mkoani Shinyanga yakiendelea.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akipima Shinikizo la damu kwenye banda la Afya.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme (katikati) akiongoza maandamano wakati wa uzinduzi wa wiki ya sheria nchini mkoani Shinyanga.
Maandamano yakiendelea.
Maandamano yakiendelea.
Mkoa wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akishiriki mazoezi.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akiangalia nyoka
 
CHANZO - SHINYANGA PRESS CLUB BLOG

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post