NEC YASHIRIKI MATEMBEZI WIKI YA SHERIA KITAIFA DODOMA

 

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele (kulia) akishiriki Matembezi ya ufunguzi wa wiki ya sheria Kitaifa Mkoani Dodoma Januari 27,2024. Matembezi hayo yaliongozwa na Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Akson na viongozi wengine mbalimbali wa Makama. Maadhimisho ya Wiki ya sharia yalianza Januari 24,2024 na yanataraji kufikia tamati Februari 1, mwaka huu. 


Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele pamoja na Mjumbe wa Tume, Mhe. Jaji (Rufaa),  Mwanaisha Kwariko ni miongoni mwa watumishi wa Mahakama walioshiriki matembezi hayo. 

Watumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakishiriki matembezi hayo.
Majaji mbalimbali wa Mahakama ya Rufaa wakiwa katika ufunguzi wa Wiki ya Sheria. 
Meza Kuu Ikiongozwa na Mgeni Rasmi, Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson wakiiamba wimbo wa Taifa.

Majaji wa Mahakama ya Rufaa wakishiriki kuimba Wimbo wa taifa na ule wa Afrika Mashariki wakati wa sherehe za ufunguzi wa Wiki ya Sheria Kitaifa iliyofanyika Januari 27,2024 katika viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma leo. 
Picha mbalimbali za pamoja. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments