Breaking : WATU ZAIDI YA 21 WAFARIKI KWA KUFUNIKWA NA ARDHI MGODINI BARIADI...RAIS SAMIA ATUMA SALAMU ZA POLE

Picha mfano wa shimo mgodini

Wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu zaidi ya 21 wamefariki dunia kufuatia ajali ya kufunikwa na ardhi katika Mgodi wa Ng'alita, Wilaya ya Bariadi, mkoani Simiyu.

Inaelezwa kuwa tukio hilo limetokea baada ya kudaiwa kuingia mgodini kwa kujipenyeza kinyume cha sheria kwani shughuli za uchimbaji zilikuwa zimesitishwa.

Kufuatia ajali hiyo iliyotokea saa 11 alfajiri Januari 13,2024 , Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pole kwa ndugu, jamaa na marafiki waliopoteza jamaa zao katika ajali hiyo na kwamba Vyombo vya ulinzi na usalama vikishirikiana na uongozi wa mkoa vinaendelea na juhudi za kutafuta miili mingine ambayo bado imekwama ndani ya kifusi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post