BABA WA SABAYA ASHINDA UENYEKITI CCM ARUSHA

 

Msimamizi wa Uchaguzi ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa Njombe Antony Mtaka amemtanganza Loy Thomas Sabaya kuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Arusha baada ya kuwashinda wenzake kwa kupata Kura 463.

Mzee Loy Thomas ni baba mzazi wa Lengai Ole Sabaya ambaye alikuwa mkuu wa wilaya ya Hai.


Uchaguzi huo ulihudhuriwa na wajumbe 907 huku waliopiga Kura hizo ni wajumbe 906, wagombea wakiwa ni wanne waliowania kinyang'anyito hicho huku Kura Moja ikiwa imeharibika.

Matokeo ya Uchaguzi wa wenyekiti Mkoa wa Arusha

Edina Kivuyo Kura 10

Solomoni Olesendeka 59

Dkt Danieli Mrisho 374

Loy Sabaya 463


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post