WAZIRI MKENDA AWATAKA WAHITIMU ADEM KUWA VIONGOZI WA MAGEUZI YA ELIMU


Na Hellen Isdory Kwavava

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema Serikali inawatarajia Wahitimu katika mafunzo ya elimu kuwa mabalozi wa utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 Toleo la 2023.

Prof. Mkenda ametoa rai hiyo Desemba Mosi, 2023, Bagamoyo Mkoa wa Pwani wakati akizungumza kwenye mahafali ya 31 ya Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM).

"Katika kipindi hiki, tunawategemea sana kwenda kutusaidia kutekeleza mageuzi ambayo yameainishwa katika Sera mpya ya Elimu, pamoja na  jukumu la kufundisha mtaenda kusimamia mabadiliko ya elimu nchini" ,amesema Prof. Mkenda.

Amesema Serikali imeanza mchakato wa mabadiliko ya Sheria ya elimu ya mwaka 1978, na kwamba kulingana na Sera Mpya ya elimu ma Mafunzo, elimu ya lazima miaka 10  badala ya miaka 7.

"Kutokana na mabadiliko ya Sera tunapitia sasa sheria ya elimu ya mwqla 1978  ili iendane na sera  pamoja na masuala  mengine muhimu, mtambuka", ameeleza Waziri Mkenda.

 Mkenda ameongeza kuwa katika Sera na Mitaala Mipya walimu watapaswa kufanya mafunzo kwa vitendo kwa muda wa Mwqka mmoja ili kujenga uzoefu kazini na kueleza kuwa matarajio ni kuwa wahitimu wq Ualimu na Uthibiti Ubora wa Shule wakiwa kazini Serikqli na jamii inawategemea sana katika kufundisha na kuwalinda wanafunzi na si viginevyo. 

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) Dkt. Siston  Masanja amesema serikali inawekeza katika mafunzo hayo ili kuwajengea Walimu umahiri  na uwajibikaji kwa Maendeleo ya nchi, hivyo wanapaswa kuwa imara na mawazo chanya katika kusimamia Shule ili kuleta mageuzi chanya yanayokusudiwa.

"Wahitimu ni nguzo muhimu ya taifa, mnapaswa kuimarisha usimamizi na utekelezaji wa miradi ya ujenzi, usimamizi wa ufundishaji na ujifunzaji, kuzingatia usalama wa watoto pamoja na miongozo mbalimbali", amesema Dkt. Masanja.

Ameishukuru Serikali kupitia Wizara ya elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kutoa fedha zinazosaidia kutekeleza ujenzi wa Kampasi ya ADEM Mbeya.

Jumla ya Wahitimu 916 wametunukiwa Stashahada, Wahitimu 702 ni wa kozi ya Stashaha ya Uongozi na Usimamizi wa Elimu (DEMA), 214 Stashahada ya Udhibiti Ubora wa Shule (DSQA) na wahitimu 03 wametunukiwa Astashahada ya Uongozi na Usimamizi wa Elimu (SELMA).

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post