WORLD VISION TANZANIA YASHIRIKI UZINDUZI KAMPENI YA 'ONGEA NAO', SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA

Mratibu wa Miradi wa Shirika la World Vision Tanzania, Wilaya ya Kishapu Yohana Masanja (kulia) akimuonesha Mgeni rasmi Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu, Fatma Mohamed (aliyevaa kiremba) mifuko ya kuchemshia maji kwa kutumia mionzi ya jua inayotolewa na Shirika kwa wananchi wilayani Kishapu ili kukabiliana na magonjwa mbalimbali. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mratibu wa Miradi wa Shirika la World Vision Tanzania, Wilaya ya Kishapu Yohana Masanja akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya ONGEA NAO na Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Shirika la World Vision Tanzania limeshiriki katika uzinduzi wa  
kampeni ya "ONGEA NAO" katika Mkoa wa Shinyanga ambayo inaratibiwa na Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania (TPF-NET) Mkoa wa Shinyanga kwa ajili utoaji wa elimu ya ukatili wa kijinsia, mauaji, mmomonyoko wa maadili kwa makundi mbalimbali lengo likiwa ni kushirikiana na jamii kutokomeza uhalifu ikiwa ni pamoja na Ukatili wa Kijinsia.

Uzinduzi wa Kampeni ya ONGEA NAO katika Mkoa wa Shinyanga imezinduliwa leo Ijumaa Desemba 1,2023 wakati wa Uzinduzi wa Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia ukiongozwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kwa kushirikiana na wadau mbalimbali uliofanyika katika shule ya Msingi Buduhe wilayani Kishapu ambapo mgeni rasmi alikuwa Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu, Fatma Mohamed.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mratibu wa Miradi wa Shirika la World Vision Tanzania, Wilaya ya Kishapu Yohana Masanja ameishukuru Serikali namna inavyoshirikiana na World Vision Tanzania katika kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto huku akisisitiza kuwa ukatili dhidi ya wanawake na watoto unatokomezwa kabisa wilayani Kishapu.

Amesema katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia World Vision Tanzania kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kupitia Dawati la Jinsia na Mtandao wa Polisi Wanawake wametoa mafunzo ya ukatili wa kijinsia katika jamii zikiwemo shule za Msingi Shiya, Lagana na Sekondari Mwakipoya.

"Sisi World Vision Tanzania tunafanya kazi kwa kushirikiana na serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhakikisha tunapinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto, ili kuhakikisha jambo hilo linatimia kikamilifu, tunazo shughuli mbalimbali tunazozitekeleza katika wilaya ya Kishapu. Miongoni mwa shughuli hizo ni utetezi wa mtoto ambapo tunahakikisha tunaunda na kujengea uwezo kamati mbalimbali kama vile MTAKUWWA, Mabaraza ya watoto na kuhakikisha yanafanya kazi kikamilifu katika kupinga ukatili dhidi ya mtoto na mwanamke",amesema Masanja.

Ameeleza kuwa pia wana shughuli za maashirio ambapo wanaungana na serikali kuinua uchumi wa kaya ambapo mwanamke ni kipaumbele chao kwa maana kwamba wanapomuinua mwanamke kiuchumi wanakuwa wamejihakikishia kuwa hatanyanyasika tena na changamoto mbalimbali zinazohusiana na unyanyasaji wa kijinsia

"Hali kadhalika tunafanya shughuli za afya pamoja na lishe na katika shughuli hizi tunaangazia afya ya mtoto katika umri wa miaka mitano na kuendelea na chini ya miaka mitano. Pia tunatoa huduma ya chakula kwa wanafunzi shuleni kwenye maeneo yetu ya miradi na tunaendelea kufanya kampeni kwa wazazi ili programu hiyo iwe endelevu kwamba mtoto anapokuwa shuleni hapati njaa, kupinga unyanyasaji maeneo ya shuleni", ameongeza Masanja kutoka World Vision ambao ni miongoni mwa wadhamini wa Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia na Uzinduzi wa Kampeni ya ONGEA NAO.

Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ambaye ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania (TPF-NET) Mkoa wa Shinyanga amewashukuru wadau mbalimbali zikiwemo asasi za kiraia kwa namna wanavyoshirikiana katika kutokomeza matukio ya ukatili wa kijinsia.

Kamanda Magomi amesema kesi nyingi za matukio ya ukatili wa kijinsia zimekuwa zikiripotiwa na kufanyiwa kazi ikiwa ni pamoja na kupelekwa mahakamani na kupata hukumu ambapo kwa sasa kuna mwitikio mkubwa wa kuripoti matukio hali inayotokana na elimu inayotolewa na Jeshi la Polisi na ushirikiano mzuri na vyombo vingine vinavyoshughulikia kesi hizi ikiwemo Mahakama, Hospitali, Idara ya ustawi wa jamii, Viongozi wa serikali za mitaa na viongozi wa dini.

"Jeshi la Polisi tunawataka wanafunzi, wananchi ,wadau kutambua kuwa mnawajibu wa kupaza sauti na kutoa taarifa za uhalifu katika vyombo vya sheria ili kukomesha vitendo hivyo katika jamii inayozunguuka, kwani jukumu la ulinzi na usalama ni la kila mwananchi",amesema Kamanda Magomi.

Mgeni rasmi Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu Bi. Fatma Mohamed ameitaka jamii kutoyafumbia macho matukio ya ukatili wa kijinsia na badala yake kila mmoja awe mstari wa mbele kutoa taarifa za matukio ya ukatili wa kijinsia ili jamii iwe salama.

Mratibu wa Miradi wa Shirika la World Vision Tanzania, Wilaya ya Kishapu Yohana Masanja akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya ONGEA NAO na Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia
Mratibu wa Miradi wa Shirika la World Vision Tanzania, Wilaya ya Kishapu Yohana Masanja (kulia) akimuonesha Mgeni rasmi Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu, Fatma Mohamed (aliyevaa kiremba) mifuko ya kuchemshia maji kwa kutumia mionzi ya jua inayotolewa na Shirika kwa wananchi wilayani Kishapu ili kukabiliana na magonjwa mbalimbali

Mratibu wa Miradi wa Shirika la World Vision Tanzania, Wilaya ya Kishapu Yohana Masanja (kulia) akimwelezea Mgeni rasmi Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu, Fatma Mohamed (aliyevaa kiremba) kuhusu shughuli zinazofanywa na Shirika la World Vision Tanzania katika kutokomeza ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ambaye ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania (TPF-NET) Mkoa wa Shinyanga akinunua asali katika banda la World Vision Tanzania
Afisa Miradi Shirika la World Vision Wilaya ya Kishapu, Enock Musa akielezea kuhusu shughuli zinazofanywa na Shirika la World Vision Tanzania katika kutokomeza ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto

Mmoja wa wajasiriamali waliowezeshwa na Shirika la World Vision namna ya kutengeneza vyakula vinanvyotokana na mazao ya lishe na ufugaji nyuki akimonesha bidhaa wanazozalisha Mgeni rasmi Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu, Fatma Mohamed na viongozi mbalimbali

Mahitaji mbalimbali yaliyotolewa kwa watu wenye uhitaji katika kaya 50 kata ya Kishapu 
Mahitaji mbalimbali yaliyotolewa kwa watu wenye uhitaji katika kaya 50 kata ya Kishapu 
Ugawaji wa mahitaji mbalimbali kwa watu wenye uhitaji katika kaya 50 kata ya Kishapu ukiendelea ambapo wamepatiwa mchele ,sabuni  sukari, maharage na mafuta ya kula.

Ugawaji wa mahitaji mbalimbali kwa wanafunzi ukiendelea ambapo wanafunzi wamepatiwa taulo za kike na madaftari

Picha ya kumbukumbu baada ya ugawaji wa mahitaji mbalimbali
Askari polisi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya ONGEA NAO na Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia

Soma pia

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post