GGML WAUNGANA NA BITEKO KUANIKA MBINU ZA MAPAMBANO DHIDI YA UKIMWI

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko (katika) akiwa na viongozi mbalimbali wa serikali pamoja na wadau wa maendeleo ikiwamo Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) ambayo iliwakilishwa na Meneja Mwandamizi wa Afya, Usalama, Mazingira na Mafunzo wa GGML, Dk Kiva Mvungi (wa kwanza kulia waliosimama) na Meneja Uhusiano na Mawasiliano, Stephen Mhando (wa kwanza kushoto waliosimama).
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko akihutubia viongozi mbalimbali wa serikali, watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI na wadau wa maendeleo ikiwamo Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) katika mkutano maalum wa wadau wanaoshughulikia udhibiti wa UKIMWI Tanzania uliofanyika juzi mjini Morogoro.


NA MWANDISHI WETU

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko amewataka wadau mbalimbali wanaohusika na mapambano dhidi ya UKIMWI nchini kwa kushirikiana na Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) kuhakikisha kuwa wanatenga fedha za kutosha kwa ajili ya mapambano dhidi ya UKIMWI nchini badala ya kutegemea wafadhili kwa kiasi kikubwa.Dk. Biteko amesema hayo jana katika mkutano maalum wa wadau wanaoshughulikia udhibiti wa UKIMWI Tanzania uliofanyika mjini Morogoro na kuhusisha viongozi wa Serikali, wanaoishi na virusi vya UKIMWI na wadau wa maendeleo ikiwamo Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML).Alisema pamoja na juhudi mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali pamoja na wadau, bado UKIMWI haujadhibitiwa inavyotakiwa, hali inayoweza kusababisha maambukizi mapya kuongezeka.Aliwataka wadau wote wanaohusika kuendelea na juhudi za utoaji afua mbalimbali zenye lengo la kutokomeza ugonjwa wa UKIMWI.“Tanzania imepiga hatua kubwa katika mapambano dhidi ya UKIMWI na nawataka TACAIDS na wadau kuhakikisha mnashirikiana kwa pamoja dhidi ya mapambano ya Ukimwi kwa kuongeza ushiriki wa wananchi pia,” amesisitiza Dk. BitekoAidha, akichangia mada katika mkutano huo, Meneja Mwandamizi wa Afya, Usalama, Mazingira na Mafunzo wa GGML, Dk Kiva Mvungi aliunga mkono hoja hizo za Dk. Biteko na kusisitiza kuwa maeneo mengine ambayo Serikali inaweza kutumia na kupunguza utegemezi wa wafadhili ni kupitia kampuni kubwa zinazofanya shughuli zake hapa nchini.“Kwa mfano GGML hushirikiana na TACAIDS kila mwaka kuandaa kampeni ya Kili Challenge ambayo washiriki hupanda na kuuzunguka mlima Kilimanjaro na fedha zinazopatikana huelekezwa katika mfuko wa kudhibiti Ukimwi pamoja na kuwezesha afua na asasi zinazojishughulisha na masuala ya Ukimwi,” alisema.Dk. Kiva alitaja mbinu nyingine ya kuondokana na utegemezi kutoka kwa wafadhili kuwa ni kushirikisha Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) ambacho kina wanachama mbalimbali wakiwamo makampuni makubwa ya madini na kampuni nyingine ambazo zitaweza kuchangia fedha za kuendeleza mapambano dhidi ya VVU/ Ukimwi.“Kwa kutumia ATE tunaweza kushirikisha wafanyakazi wetu au kuwatia moyo wanachama wa ATE wawe na mtazamo na kusaidia jamii na kufanya tathmini ya mahali ambapo mtu au kampuni husika inapofanya kazi. Kisha tunaingia kwenye jamii za kupima kama kweli huduma hizo muhimu za elimu ya afya zimetolewa.Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dk. Jerome Kamwela alisema mkutano huo unalenga kutoa nafasi ya mashaurinao kati ya Serikali na wadau wake katika mapambano dhini ya UKIMWI.Alisema mkutano huo ni muhimu hasa wakati huu ambao Tanzania inaelekea kufikia lengo la dunia la kumaliza UKIMWI ifikapo mwaka 2030.“Lengo linataka kusiwe na maambukizi mapya ya UKIMWI, kusiwe na vifo vinavyotokana na UKIMWI pia, kusiwe na unyanyapaa kwa watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi,” alisema.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post