WAZIRI BASHUNGWA AWATAKA TANROAD KUWASIMAMIA KWA UMAKINI WAKANDARASI WANAOTEKELEZA MIRADI NCHINI

WAZIRI wa Ujenzi Inocent Bashungwa kushoto  akikagua barabara inayotoka Kwamsisi kuelekea Pangani mkoa ni Tanga wakati wa ziara yake kulia ni Mkuu wa wilaya ya Handeni Albart MsandoWaziri wa Ujenzi Inocent Bashungwa akizungumza mara baada ya kuikagua barabara hiyo kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Handeni Albarto Msando

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Handeni Saitoti Zelothe akizungumza wakati wa ziara hiyo kulia ni Waziri wa Ujenzi Inocent Bashungwa
Na Oscar Assenga,HANDENI


WAZIRI wa Ujenzi Inocent Bashungwa ameiagiza Wakala wa Barabara nchini (TANROAD) kuhakikisha wanawasimamia kwa umakini wakandarasi wanaotekeleza miradi ya barabara nchini kutokana na kusuasua na serikali kutoridhishwa na kasi ya ujenzi.Sanjari na agizo hilo pia amesema iwapo miradi hiyo ya barabara itaendelea kusuasua atalazimika kumshauri Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ambadilishe Mtendaji Mkuu wa Tanroad nchini Mohamed Besta kama ataendelea kucheka na wakandarasi hao bila ya kuwachukulia hatua.Bashungwa aliyasema hayo leo wakati wa ziara yake ya siku moja wilayani Handeni na Pangani ambapo alikagua barabara ya kutoka Tanga-Pangani hadi Bagamoyo ambayo inatekelezwa na mkandarasi wa kampuni ya Kichina ya Railway 15, hakuridhishwa na kasi ya ujenzi wake.Alisema kwamba kuna miradi mingi imekuwa ikisuasa suasua lakini bado wanaendelea kuiangalia bila kuchukua hatua jambo ambalo linakwamisha juhudi kubwa za Serikali kuifungua nchi kupitia miradi ya barabara ya kimkakati.“Barabara hii nikuambie Mkurugenzi Mkuu wa Tanroad, kama hatutachukua hatua kwa muda unaotakiwa miradi kama hii inayoendelea kusuasua nitamshauri rais akubdilishe hatuwezi kuendelea namna hii”Alisema Waziri Bashungwa.“Lakini pia Kaimu Mkurugenzi wa Miradi Tanroad tumemuamini tumekukaimisha ili usimamie hayo tumekuwa na wewe uone, Boniface Mkumbo yule aliyekuwa kabla yako nilipokuja kumtoa ilikuwa mbinde kwa sababu ya kulindana sasa Mkurugenzi Mtendaji baada ya wao utakuwa wewe kama usipobadilika”AlisemaWaziri huyo alisema haiwezekani anapokwenda kila kipande cha barabara nchini niwaamshe nyie hapana lazima mbadilike kama sijawaamsha na ile mipango mlioniambia naenda kukagua barabara lakini sitaki wakandarasi wa aina hii kule yule CR 7 hawa ni CR 15 wanaweza kukuta mtu na binadamu yake.“Lakini yule CR 7 ni shida kwani miradi kama sita imesimama kwa sababu ya kurundikiwa miradi na nyie mnajiita CR 15 nyie mnauhusiana na C7 hii ni tatizo kila mradi mnaoufanya hii barabara wananchi mmesikia mipango ya Serikali ninakwenda kuikagua”AlisemaAliwaambie wananchi tayari Serikali imeshaleta fedha lakini mkandarasi anawachelewesha wameona ni kwanini wanawachelewesha Mkurugenzi wa barabara hautakiwa kuwa ofisini unapaswa uzungumze maeneo mbalimbali nchini ili uweze kuona changamotoAwali akizungumza wakati wa ziara hiyo Mtendaji Mkuu wa Tanroad alimueleza Waziri Bashungwa kwamba hatua ambazo wamechukua ni kumuelekeza mkandarasi aongeze vifaa na awe na mpango kazi ambao unaendana na wakati.Alisema kwa sababu kwa sasa yupo nyuma ya asilimia 19 ya mpango wake ya kazi na Novemba 14 waliwaita makao makuu na kukaa kikao nao na baadae Novemba 28 wamewaita tena ili kuona kama yale maelekezo yametekelezwa.Naye kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Handeni Albert Msando alisema kwamba wananchi wa eneo la Kwamsisi wameandika Historia kwa kuwa Waziri wa kwanza kufikia na kuzungumza nao na kutembelea barabara hii na wananchi walikuwa wamekata tamaa.Alisema kwamba wanawaomba wanapokwenda kwa maofisi ya wakuu wa wilaya wasije na kuondoka na waache kujifungia ofisini wabadilike watumie ofisi zilizopo katika maeneo wanayotekeleza miradi.“Mh Waziri sisi hapa leo tunapoteza tuna mazao mengi tunalima unaweza kukaa wiki nzima hautaja toa mazao na hivyo kupoteza mapato mengi ambayo serikali yangepatikana kwamsisi jana na juzi wamekusanya 0 hakuna gari zinaingia shambani kwa sababu ya ubovu wa barabara”AlisemaAlisema kwa sababu wao ni wazalishaji wengi ya muhogo barabara hii itakuwa mkombozi na wananchi hao watakukuyumbisha hivyo Tanroad lazima waangalie mahitaji ya wananchi na fedha imetengwa haenda hatua moja mbele.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post