TBS YAADHIMISHA SIKU YA UBORA NA KUTOA TUZO

Mkurugenzi wa Maendeleo ya Viwanda  kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara  Bw.Sempeho Nyari akizungumza katika Maadhimisho ya kilele Cha wiki ya Ubora ambayo yameambatana na utoaji Tuzo za Ubora ambazo zimetolewa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) yaliyofanyika leo Novemba 9, 2023 katika Ukumbi wa Maktaba Mpya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

MKURUGENZI wa Maendeleo ya Viwanda  kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara  Bw.Sempeho Nyari amewataka wazalishaji wa bidhaa nchini na watoa huduma kutoka sekta za umma na binafsi kuunda miundombinu ambayo itasaidia kuzalisha bidhaa na huduma zenye ubora ili kuweza kushindana katika Soko la kimataifa.

Ameyasema hayo leo Nov 10,2023 Jijini Dar es Salaam katika Maadhimisho ya kilele Cha wiki ya Ubora ambayo yameambatana na  utoaji Tuzo za Ubora ambazo zinatolewa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) yaliyofanyika katika Ukumbi wa Maktaba Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

Amesema miundombinu ya ubora ni moja ya mambo muhimu yanayo changia katika kukuza uchumi na maendeleo ya Viwanda na Biashara  nchini kwa kuzalisha bidhaa na huduma zenye ubora.

“Maadhimisho ya wiki ya Ubora duniani mwaka huu yamebeba kauli mbiu ambayo tumeielekeza ambayo inazungumzia  UBORA TAMBUA UWEZO WAKO WA KUSHINDANA, kauli mbiu hii imekuja wakati muafaka kwa Tanzania hususani katika kipindi hiki ambapo ni moja ya nchi ambayo imeingia katika soko huru la biashara Afrika, soko hili ni  kubwa sana ambalo linahitaji sana bidhaa ambazo zina Ubora na huduma zilizofunikwa na ubora wa juu ili kulifikia kwa ukamilifu"Amesema

Aidha Bw.Sempeho amesema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara ilitambua ni muhimu kuanzisha Tuzo za Ubora za Kitaifa ambazo zitaratibiwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa kushirikiana na ZBS pamoja  Sekta binafsi na wadau wengine ili kuhakikisha bidhaa na huduma zinazotolewa zinakidhi ubora Kitaifa,kikanda na Umoja wa Afrika mashariki ili tuweze kulifikia soko.

"Nchi yetu ni moja ya nchi ambayo ipo kwenye Umoja wa kikanda yaani SADC na Umoja wa Afrika Mashariki EAC na Sasa hivi tumeingia soko huru la Afrika ni matumaini yangu tukizingatia zana ya ubora tutaingia sokoni kama washindani". Bw.Sempeho ameeleza. 
 
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi(TBS) Prof. Othman Chande ametoa wito kwa wazalishaji kuendelea kuzalisha bidhaa bora kila mwaka ili kuwa na utofauti kwa uboreshaji Viwango ili kukidhi mahitaji ya Soko.

Naye Mkurugenzi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Dkt Athuman Ngenya amesema wiki ya Ubora inamanufaa makubwa kwetu kwani itasaidia kuhamasishana kutengeneza bidhaa zenye ubora katika kushindana kwenye Soko la kimataifa.

"Tanzania sio kisiwa ili kunyanyua maisha ya Wananchi wetu lazima tutengeneze, lazima tuingie katika Ushindani ukienda soko hafumbi tu macho anaangalia unakua unachagua kipi ni bora  na kipi sio bora, wiki hii imekuja ili kukumbushana  juu ya kuhakikisha bidhaa zetu zinatengenezwa kwa ubora". Amesema Dkt.Ngenya

Tuzo hizo za Ubora  zimetolewa kwa Mara ya kwanza mwaka 2020/ 2021 ambapo hakukuwa na mwamko mkubwa katika Ushindani,washindi ambao wamepatikana katika Tuzo za 2022/2023 watapata fursa ya kufahamika nchini na kushiriki katika mashindano ya Tuzo za Ubora Afrika mashariki na ukanda wa SADC.

Mkurugenzi wa Maendeleo ya Viwanda  kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara  Bw.Sempeho Nyari akizungumza katika Maadhimisho ya kilele Cha wiki ya Ubora ambayo yameambatana na utoaji Tuzo za Ubora ambazo zimetolewa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) yaliyofanyika leo Novemba 9, 2023 katika Ukumbi wa Maktaba Mpya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Viwanda  kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara  Bw.Sempeho Nyari akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la TBS katika Maadhimisho ya kilele Cha wiki ya Ubora ambayo yameambatana na utoaji Tuzo za Ubora ambazo zimetolewa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) yaliyofanyika leo Novemba 9, 2023 katika Ukumbi wa Maktaba Mpya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Viwanda kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara  Bw.Sempeho Nyari akimsikiliza mmoja wa wajasiriamali alipotembelea mabanda ya wajasiriamali katika Maadhimisho ya kilele Cha wiki ya Ubora ambayo yameambatana na utoaji Tuzo za Ubora ambazo zimetolewa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) yaliyofanyika leo Novemba 9, 2023 katika Ukumbi wa Maktaba Mpya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Viwanda kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara  Bw.Sempeho Nyari akiwa pamoja na watumishi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wakitembelea mabanda ya wajasiriamali katika Maadhimisho ya kilele Cha wiki ya Ubora ambayo yameambatana na utoaji Tuzo za Ubora ambazo zimetolewa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) yaliyofanyika leo Novemba 9, 2023 katika Ukumbi wa Maktaba Mpya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi(TBS) Prof. Othman Chande akizungumza katika Maadhimisho ya kilele Cha wiki ya Ubora ambayo yameambatana na utoaji Tuzo za Ubora ambazo zimetolewa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) yaliyofanyika leo Novemba 9, 2023 katika Ukumbi wa Maktaba Mpya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Dkt Athuman Ngenya akizungumza katika Maadhimisho ya kilele Cha wiki ya Ubora ambayo yameambatana na utoaji Tuzo za Ubora ambazo zimetolewa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) yaliyofanyika leo Novemba 9, 2023 katika Ukumbi wa Maktaba Mpya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Meneja Ithibati Ubora wa Bidhaa, Bi. Amina Yassin akizungumza katika Maadhimisho ya kilele Cha wiki ya Ubora ambayo yameambatana na utoaji Tuzo za Ubora ambazo zimetolewa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) yaliyofanyika leo Novemba 9, 2023 katika Ukumbi wa Maktaba Mpya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa la Ubora Tanzania Bw.Safari Fungo akizungumza katika Maadhimisho ya kilele Cha wiki ya Ubora ambayo yameambatana na utoaji Tuzo za Ubora ambazo zimetolewa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) yaliyofanyika leo Novemba 9, 2023 katika Ukumbi wa Maktaba Mpya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Matukio mbalimbali ya makabidhiano ya tuzo katika Maadhimisho ya kilele Cha wiki ya Ubora ambayo yameambatana na utoaji Tuzo za Ubora ambazo zimetolewa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) yaliyofanyika leo Novemba 9, 2023 katika Ukumbi wa Maktaba Mpya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Viwanda kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara  Bw.Sempeho Nyari (katikati) akipata picha ya pamoja na washindi wa Tuzo za Ubora katika Maadhimisho ya kilele Cha wiki ya Ubora ambayo yameambatana na utoaji Tuzo za Ubora ambazo zimetolewa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) yaliyofanyika leo Novemba 9, 2023 katika Ukumbi wa Maktaba Mpya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post