KATIBU MKUU WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA AWATAKA WADAU WA VIWANGO KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO TBS

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt.Hashil Abdallah akimkabidhi cheti cha utambuzi Mwenyekiti wa Bodi ya TBS, Prof.Othuman Chande katika hafla ya Maadhimisho ya Siku ya Viwango Duniani leo Novemba 30,2023 kwenye Ofisi za TBS Jijini Dar es Salaam.

***************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt.Hashil Abdallah amewataka wadau wa viwango kuendelea kushirikiana na Shhirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa kutoa msaada na uzoefu katika taaluma zao kwa kuchangia ipasavyo katika utengenezwaji wa viwango hapa nchini.

Ametoa wito huo leo Novemba 30,2023 Wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Viwango Duniani kwenye Ofisi za TBS Jijini aDar es Salaam ambapo amesema kuna umuhimu mkubwa kwa wadau wote na wananchi kwa ujumla kushiriki na kutoa maoni katika mchakato wa uandaaji na utengenezaji viwango ili vikidhi mahitaji ya jamii.

"Uandaaji wa viwango unashirikisha watu wote kwa pamoja na uwepo wa viwango utahakikisha usalama, afya na ubora wa bidhaa katika jamii yetu". Amesema Dkt. Abdallah.

Aidha amesema kuwa Maadhimisho ya Siku ya Viwango Duniani ni muhimu kwani ni njia mojawapo ya kuenzi juhudi shirikishi za maelfu ya wataalamu duniani kote ambao hutengeneza mikataba ya hiari na lazima ya kiufundi ambayo huchapishwa kama viwango vya kitaifa na kimataifa ili kulinda afya za walaji na mazingira.

Amesema Shirika la viwango Tanzania linafanya kazi kwa kushirikiana kwa karibu na wadau mbalimbali katika kuendeleza sekta ya viwanda na biashara na kusimamia viwango kwa bidhaa zinazozalishwa hapa nchini.

"Nawashukuru wadau wote wakiwemo taasisi za elimu ya juu, taasisi za utafiti, mashirika ya umma, wadau wa maendeleo, wazalishaji, wajasiriamali na vyama vya kisekta kwa kuendelea kuandaa viwango kwa ufanisi mkubwa". Amesema

Pamoja na hayo amesema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wazalishaji, wafanyabiashara na wenye viwanda ili kukuza uchumi wa nchi yetu, ikiwa ni pamoja na kusimamia maendeleo ya viwango na ubora wa bidhaa zinazozalishwa katika sekta mbalimbali na viwandani.

"Sekta ya viwanda na biashara ni moja ya mihimili mikubwa katika kukuza uchumi wa nchi yetu na kuchangia katika pato la taifa kutokana na bidhaa za viwandani zinazozalishwa na kuuzwa ndani na nje ya nchi, pamoja na kutoa ajira kwa Watanzania". Ameeleza

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt. Athuman Ngenya amesema kuwa maadhimisho hayo yalianza kufanyika October 9 hadi 13, 2023 kwa shughuli mbalimbali za kuelimisha umma kupitia vyombo vya Habari na mitandao ya kijamii juu ya umuhimu wa kushiriki katika mchakato wa uandaaji wa viwango vya kitaifa, kikanda na kimataifa.

Amesema kuwa TBS, kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, imefanikiwa kuandaa viwango zaidi ya 4,000 ambavyo ni pamoja na vile vinavyobainisha matakwa ya usalama, matakwa ya utengenezaji, matakwa ya matumizi pamoja na kanuni za upimaji ambapo vyote vikiwa na lengo la kuboresha bidhaa na huduma.

Katika kuelekea maadhimisho ya siku ya (African Organization for Standardization) ARSO Afrika inayotegemewa kufanyika mwezi Machi 2024, Katibu Mkuu Dkt. Abdallah amezindua mashindano ya uandishi wa insha kwa wanafunzi wa vyuo vikuu yenye kauli mbiu isemayo “Empowering consumers through Standardization to achieve their rights to safe Quality Good &Services”.

Mashindano hayo yamelenga kuwapata washindi katika ngazi ya kitaifa ili waweze kushiriki katika ngazi ya kikanda na hatimaye kupata mshindi katika bara la Afrika kwa ujumla.
 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt.Hashil Abdallah akiwakabidhi vyeti vya utambuzi wadau wa Viwango katika hafla ya Maadhimisho ya Siku ya Viwango Duniani leo Novemba 30,2023 kwenye Ofisi za TBS Jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt.Hashil Abdallah akiwakabidhi vyeti vya utambuzi wadau wa Viwango katika hafla ya Maadhimisho ya Siku ya Viwango Duniani leo Novemba 30,2023 kwenye Ofisi za TBS Jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt.Hashil Abdallah akiwakabidhi vyeti vya utambuzi wadau wa Viwango katika hafla ya Maadhimisho ya Siku ya Viwango Duniani leo Novemba 30,2023 kwenye Ofisi za TBS Jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt.Hashil Abdallah akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mashindano ya uandishi wa insha kwa wanafunzi wa vyuo vikuu yenye kauli mbiu isemayo “Empowering consumers through Standardization to achieve their rights to safe Quality Good &Services” katika hafla ya Maadhimisho ya Siku ya Viwango Duniani leo Novemba 30,2023 kwenye Ofisi za TBS Jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt.Hashil Abdallah akizungumza na wadau wa Viwango katika hafla ya Maadhimisho ya Siku ya Viwango Duniani leo Novemba 30,2023 kwenye Ofisi za TBS Jijini Dar es Salaam .
Mwenyekiti wa Bodi ya TBS, Prof.Othuman Chande akizungumza na wadau wa Viwango katika hafla ya Maadhimisho ya Siku ya Viwango Duniani leo Novemba 30,2023 kwenye Ofisi za TBS Jijini Dar es Salaam .
Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt. Athuman Ngenya akizungumza na wadau wa Viwango katika hafla ya Maadhimisho ya Siku ya Viwango Duniani leo Novemba 30,2023 kwenye Ofisi za TBS Jijini Dar es Salaam .
Wadau wa Viwango wakiwa katika hafla ya Maadhimisho ya Siku ya Viwango Duniani leo Novemba 30,2023 kwenye Ofisi za TBS Jijini Dar es Salaam .
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt.Hashil Abdallah akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau wa Viwango katika hafla ya Maadhimisho ya Siku ya Viwango Duniani leo Novemba 30,2023 kwenye Ofisi za TBS Jijini Dar es Salaam .
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt.Hashil Abdallah akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau wa Viwango katika hafla ya Maadhimisho ya Siku ya Viwango Duniani leo Novemba 30,2023 kwenye Ofisi za TBS Jijini Dar es Salaam .

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post