KAIMU NAIBU MRATIBU MKUU WA MASUALA YA UKIMWI WA PEPFAR NCHINI MAREKANI ATEMBELEA SHUGHULI ZINAZOTEKELEZWA KUPITIA UFADHILI WAOKAIMU Naibu Mratibu Mkuu wa Masuala ya Ukimwi wa mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Ukimwi (PEPFAR) Dkt Rebbeca Bunnell na ujumbe wake wamefanya ziara ya kutembelea katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo akiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt Grace Magembe.

Akiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo walitembelea shughuli zinazotekelezwa kupitia ufadhili wa PEPFAR kupitia kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa cha Marekani (CDC) kinachosaidia upatikanaji wa baadhi ya huduma katika Hospitali hiyo huku akiridhishwa na huduma zinazotolewa.

Kupitia PEPFAR, CDC ilianza kusaidia Asasi ya Kiraia ya Gift of Hope Foundation mwaka 2019 ili kuwezesha huduma za kinga miongoni mwa vijana walioathirkka na matumizi ya dawa zaa kulevya na kusaidia upatikanaaji wa huduma za afya kwa watu wanaojidunga kutumia dawa za kulevya.

Hadi kufikia Octoba 2023,The Gift Of Hope Foundation imesaidia zaidi ya wapokea huduma 365 kupata Methadone katika kliniki ya waraibu wa dawa za kulevya (MAT) ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo huku wateja 22 wakiwa katika nyumba ya kusaidia kuacha matumizi ya dawa za kulevya (Sober House).

The Gift Of Hope pia imepanua huduma zake ili kutoa msaada wa kisaikolojia –kijamii na huduma za uhamasishaji,ikijumuisha kukaa kwa muda waa miezi mitatu katika Sober House kwa wapokea huduma wakati wanaahudhuria kliniki za MAT ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo.

Katika ujumbe wake pia wametembelea kliniki ya tiba saidizi ya Methadone (MAT) na kupata taarifa juu ya huduma za tiba na matunzo kwa watu wanaoishi na VVU (WAVIU) zikiwemo huduma za uchunguzi na matibabu ya kifua kikuu,homa ya Ini B na C na uchunguzi wa ukatili wa kijinsia.

Kliniki hiyo ya MAT ilianzishwa mwaka 2020 na hadi kufikia Septemba mwaka huu ilikuwa imewaahudumia jumla ya wapokea huduma 959 kati yao wanawake 27 na wanaume 932 ambapo hiyo ni kliniki pekee ya MAT mkoani Tanga.

“Kliniki hii inatoaa huduma za kina za kuzuia VVU pamoja na tiba matunzo, huduma za kifua kikuu, huduma za msaada wa kisaikolojia na kijamii na uibuaji wa watu wanaojidunga /kutumia dawa zaa kulevya ...The Gift of Hope ni mojawapo ya Asasi za Kiraia zinazoibua na kuunganisha wateja na matibabu katika kliniki ya MAT”

Dkt Bunnell pia ametembelea kliniki ya tiba na matunzo ya VVU (CTC) na kupata taarifa juu ya huduma jumuishi ya tiba na matunzo kwa watu wanaoishi na VVU ikiwa ni pamoja na ujumuishaji wa huduma za uchunguziz wa saratani ya mlangio wa kizazi.

Ambapo hadi kufikia Octoba 2023 kituo hicho kilikuwaa na zaidi ya wapokea huduma 2,700 waliosajiliwa katika huduma za dawa zaa kufubaza makali ya VVU (ART).

Kwa kipindi cha Octoba 22 hadi Septembea 2023 wanawake 1,287 wanaopataa huduma zaa tiba na matunzo katika kliniki hiyo walifanyiwa uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi ambapo 47 sawa ana asilimia 3.65 walibainika kuwa na viashiria vya awali vya saratani yaani VIA Positive,na 38 walitibiwa kwa tiba Mgandisho (cryotherapy) .

Ambapo wapokea huduma 23 walihisiwa kuwa na saratani ya mlango wa kizazi na walifaanyiwa uchunguzi wa kina na kumi na sita kati yao walithibitishwa kuwa na saratani ya mlango wa kizazi.

Ujumbe huo pia utaelezwa kuhusu shughuli za chanjo ya Human Papillomavirus (HPV) zinazofaanywa katika kituo hicho huku ikieleza walikuwa na wasichana 27 waliostahili kupata chanjo hiyo na walisimamia wasichana 26 kati yao 21 walikamilisha dozi tatu za HPV,wasichana watano wakiwa bado kwenye ratiba ya kupata dozi ya pili.

Kadhalika Dkt Bunnell amepataa fursa ya kuzungumza na vijana rika balehe wa kike na kiume wanaopatiwa huduma tiba na matunzo katikaa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga ili kujifunza wanavyonufaika na afua zinazofadhiliwa na PEPFAR na CDC Hospitalini hapo.

Hata hivyo pia Dkt Bunnell ametembelea maabara hya Hospitali hiyo na kushuhudia uchakataji wa sampuli za damu iliyo kaushwa (DBS) na makohozi kwa ajili ya kipimo cha kifua kikuu na kuelezwa jinsi ambavyo sampuli za wingi wa VVU huchakatwa ili kusafirishwa kwa upimaji kwenye maabaraa husika.

Kwa sasa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga inapokea Ufadhili wa PEPFAR/CDC kupitia Shirika lisilo la Kiserikali la Tanzania Healthe Promotion Support (THPS).

Tanzania Health Promotion Support (THPS) ni Taasisi ya Kitanzania iliyoanzishwa mwaka 2011 kwa kufuatia Sheria ya Mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali Na 24 hya mwaka 2002.

THPS inatekeleza kazi zake kwa kushirikiana na Wizara ya Afya,Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalumu,Wizara ya Maendeleo ya Jamii ,Jinsia,Wazee na Watoto ,Ofisi ya Rais -Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Wizara ya Mambo ya Ndani na Wizara ya Afya huko Zanzibar.

Lengo la THPS ni kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora za afya kwa watanzania ,kupitia uimarishwaji wa mifumo ya afya na jamii ili kutoa huduma bora za afya zikiwemo za VVU na UKIMWI,Kifua Kikuu,Kuzuia ukatili wa Kijinsia,Afya ya Mama na Mtoto ,Afya ya Uzazi na Afya ya Vijana  ikiwemo kuboresha mifumo ya maabara na Taarifa za Afya,Uviko 19 na Tafiti za Afya ya Jamii

Mradi wa CDC/PEPFAR Afya hatua (octoba 2021 hadi Septemba 2026) umelenga kutoa huduma jumuishi, katika vituo vya Afya (Kigoma, Pwani, Shinyanga na Tanga) na katika jamii (Kigoma, Pwani na Tanga) huduma za Kinga, matibabu na matunzo ya VVU zikiwemo huduma za kitabibu za Tohara kwa wanaume katika mikoa ya Kigoma na Shinyange na Programu ya Dreams kwa wasichana balehe na wanawake wadogo katika mkoa wa Shinyanga

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post