SERIKALI YAWATAKA WAHITIMU KUCHANGAMKIA FURSA ZA KIUCHUMI KATIKA SEKTA YA UFUGAJI NYUKINa. John Bera - Tabora

Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imewataka wahitimu wa sekta ya nyuki wa Chuo cha Mafunzi ya ufugaji nyuki Tabora (BTI), kuwa wabunifu na kutumia fursa zilizo katika mnyororo wa zao hilo ili kujiajiri.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Kitengo cha Mafunzo na Utafiti wa Wizara ya maliasili na Utalii, Dk Edward Kohi ambaye amemwakilisha Katibu Mkuu katika maafali ya 12 ya Chuo hicho  cha Mafunzo ya Ufugaji Nyuki ambapo amesema Wizara itaendelea kutoa nafasi za ajira kwa kadri upatikanaji wa vibali vya kufanya hivyo.

"Kinachotakiwa ni kuwa wadadisi wa fursa zilizopo katika mnyororo mzima wa thamani katika sekta ya ufugaji nyuki, Nina imani hamuwezi kukosa nafasi katika mnyororo huu." amesema Dkt. Kohi


Aidha, Dkt. Kohi amesema mpaka sasa Serikali imeendelea kuweka mazingira wezeshi na kuwajengea uwezo wadau mbalimbali katika kusimamia rasilimali za nyuki na kuendelea kukuza mchango wake katika pato la taifa ikiwa ni pamoja na kukuza uzalishaji wa mazao ya nyuki nchini.
.
Amesema Serikali imeanzisha  Mkakati wa wananchi wote kuachia shoka na kukakamata mzinga lengo ikiwa ni kuboresha sekta ya ufugaji nyuki hivyo wahitimu hao watumie fursa hiyo kubuni na kuanzisha kampuni za kufanya biashara ya ufugaji nyuki.

"Wizara inaendelea na Mkakati wake nchi nzima wa kuachia shoka na kukamata mzinga, Tumieni fursa hii kuanzisha kampuni za kuwasaidia kufanya biashara katika sekta ya ufugaji nyuki" Alisema Dkt. Kohi 

Ameongeza kuwa serikali inaendelea kubuni mbinu mbalimbali za kukuza sekta ya misitu na nyuki na kuendelea kuboresha mnyororo wake wa thamani ili kila mshiriki katika mnyororo huu uweze kufaidika.

"Nia ya serikali ni kukuza sekta ya misitu na nyuki ili iweze  kuleta  tija zaidi,  Hivyo niendelee kuwatia moyo kuwa serikali ina nia njema ya kukuza na kusimamia seka hii ya ufugaji nyuki."

Sambamba na hayo, Dkt. Kohi ameongeza kuwa Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii lengo lake kuu nikuona vyuo mbalimbali vilivyopo chini ikiwemo Chuo cha Mafunzo ya Ufugaji Nyuki (BTI) kinatoa elimu bora ikiwemo kuwa na waalimu wenye weledi katika sekta hiyo.

Vilevile amesema lengo lingine nikuhakikisha vyuo hivyo vinatengeneza mahusiano na Taasisi mbalimbali za nje ili kuongeza uelewa na weledi.

Sanjari na hayo, Amewataka wakazi wa Tabora   kujiandaa na kongamano lijalo la Ufugaji nyuki la "Apimondia" linalo tarajia kufanyika mwaka 2027 kutengeneza fursa za kujipatia kipato kupitia kongamano hilo

Aidha, Aliongeza kuwa katika kutatua changamoto za malazi katika chuo hicho, Wizara kupitia Mradi wa BEVAC imepanga kujenga Bweni la wanafunzi  wa kike mia tatu (300) huku Bweni la Wavulana likiwa katika mkakati pia.

Kwa Upande wake Mkuu wa Chuo Cha Mafunzo cha Ufugaji Nyuki ( BTI),  Semu Daud amesema jumla ya wahitimu waliyohitimu chuoni hapo ni  243 ambapo kwaupande wa  Shahada   jumla ni wahitumu 114 na Astashahada ni wahitimu 129.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post