WANANCHI WATAKIWA KUPATA ELIMU YA KUTOSHA YA MIKOPO KABLA YA KUCHUKUA


Meneja Masoko na Uhamasishaji wa Mfuko wa Self Microfinance Fund uliopo chini ya Wizara ya fedha Linda Mshana akiongea na waandishi wa habari katika Maonesho ya tatu ya wiki ya Huduma za Kifedha Kitaifa yanayofanyika mkoani Arusha, kwenye viwanja vya Sheikh Amri Abed Jijini, Arusha
Afisa mikopo kutoka  Self Microfinance Fund 
Mbwana Msangule akiendelea kuwapa elimu wateja waliouthuria katika banda lao lililopo katika Maonesho

Na Woinde Shizza , ARUSHA


Ili kuepuka matatizo ya kuuziwa mali , kutokana na kushindwa kurejesha mikopo wanayochukua katika taasisi mbalimbali watanzania wametakiwa kujitokeza Kwa wingi kupata elimu itakayowasaidia kutimiza malengo yao ambayo yatasaidia kukuza uchumi wao pamoja na nchi kwa ujumla.


Aidha pia kutokuwa na uelewa wa kutosha pamoja na elimu ya duni ndio chanzo pekee kinachopelekea baadhi ya watanzania kushindwa kurejesha mikopo mbalimbali kwani watu wengi wamekuwa wakifanya maamuzi pasipo kuwa na uelewa wa kutosha katika eneo hilo.


Hayo yamebainishwa na Meneja Masoko na Uhamasishaji wa Mfuko wa Self Microfinance Fund uliopo chini ya Wizara ya fedha Linda Mshana wakati akiongea na waandishi wa habari katika Maonesho ya tatu ya wiki ya Huduma za Kifedha Kitaifa yanafanyika mkoani Arusha, kwenye viwanja vya Sheikh Amri Abed Jijini, Arusha ambapo alisema kuwa mfuko huo umelenga kukidhi mahitaji ya mikopo kwa makundi mbalimbali Tanzania


Alisema kuwa kumekuwa na tatizo la wananchi wengi kuchukua mikopo bila kupata elimu ya kutosha ya namna ya kurejesha mikopo hiyo ,asilimia wanayopaswa kurejesha na namna ya kutumia mikopo hiyo katika lengo kusudiwa
Alisema kuwa mfuko huo pia unasaidia kutatua matatizo ya wananchi katika mahitaji ya msingi katika kukuza ujasiriamali, biashara, Kilimo ,Ufugaji vilevile hata kupata makazi na kuwekeza kwenye viwanda.


Alibainisha kuwa kulingana na mahitaji ya mikopo na kuongezeka kwa utitiri wa taasisi za mikopo,vijana wa kitanzania wanashauriwa kuungana na kukopa kwenye taasisi za fedha za kuaminika na zenye usimamizi wa serikali ili kuepuka fedhea katika mikopo hiyo huku akiwasihi kupata elimu ya kutosha kabla ya kuichukuwa mikopo hiyo .

Alitaja aina za mikopo ambazo zinatolewa na mfuko wa SELF Microfinance ni pamoja na mkopo wa Kilimo,Biashara, Makazi,mkopo wa Pamoja, mkopo wa Imarika, Mkopo wa Mahitaji na mikopo wa Mkulima ambapo pia alifafanua kuwa nia yao ni kuendela kuwapatia watanzania elimu na kuchangamkia fursambalimbali zilizopo hapa nchini.

Alisema kuwa kila mtanzania ana fursa kubwa ya kupata mkopo na kujikuza kiuchumi, kwa wajasiriamali wote wachini, wa kati, wakubwa, wafanyakazi,na watuwanaotaka kuboresha makazi.

“Wale waliopo kwenye vikundi wanaotaka mikopo ya kujiinua kiuchumi, wasiache fursa zikawapita, tunawafanyakazi waliokidhi na wana weledi wakuhudumia wajasirimali wote wanaotaka kujinua kichumi wafike tu katika matawi yetu yalipo katika mikoa mbalimbali ikiwemo hapa Arusha katika jengo la hazina ,Mwanza ,Dodoma,Dar es salaam ,Mbeya, Kahama ,Geita, Morogoro,Tanga ,Mtwara, Iringa pamoja na Zanzibar kupata elimu ya kutosha kuhusiana na mikopo namna ya kurejesha pamoja na riba" ,alibainisha Linda.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post