WAZIRI NAPE AIONGOZA TTCL KUZINDUA HUDUMA YA WI-FI BENJAMIN MKAPA

 


Na Mwandishi wetu Dar es salaam

Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limetekeleza maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan la kutaka uwanja wa Benjamin Mkapa uwekewe huduma ya Mtandao yaani Inteneti ikiwa ni sehemu ya ukarabati katika uwanja huo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo ya Mtandao katika uwanja huo leo Novemba 5,2023 Waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe.Nape Nnauye amesema kutekelezwa kwa agizo hilo la Dkt.Samia linakwenda kuwasaidia mashabiki wote wanaoingia kutazama mpira kufurahia kwa kutumia mtandao wenye kasi zaidi.


“Leo tunaanza kuzindua huduma hii ya mtandao wenye kasi katika Uwanja huu wa Mkapa na kwa maagizo ya Rais Samia ni kwamba viwanja vyote vipate huduma ya mtandao ili wanaohudhuria viwanjani wafurahie Mtandao,” amesema Nape

Katika hatua nyingine Mhe.Nape amelipongeza Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) chini ya Mkurugenzi wake Mhandisi Peter Ulanga kwa kufanikisha uwekaji wa huduma hiyo katika uwanja wa Benjamin Mkapa.

“Pigeni makofi ya kutosha kwa TTCL kwa kufanikisha hili la kuweka huduma hii ktaika uwanja huu na naamini kiwanja hiki ni ch kwanza na viwanja vingine vitafuata sasa mnawafanya mashabiki wafurahie kuja uwanjani kwa sababu wanafurahia huduma ya mtandao ambao nimefanyia majaribio na una kasi kwelikweli,”amesema Nape

Nape ameipongeza Azam Media Kwa kuendelea kurusha Matangazo ya mpira Kwa ubora Huku akiamini kuwa uwepo wa Mtandao WA uhakika kutoka TTCL itaendelea kunogesha Matangazo yao.

Hafla hiyo pia imeshuhudiwa na Naibu Waziri Mhe. hamis Mwinjuma, Katibu mkuu Bw. Gerson Msigwa Naibu katibu Mkuu Bw. Nicholas Mkapa Mkurugenzi mkuu wa TTCL Mhandisi Peter ulanga mashabiki pamoja na wapendasoka waliojitokeza uwanjani hapo kushuhudia mechi ya watani wa jadi Simba na Yanga.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post