HARAKATI NGAZI YA JAMII ZIMEBADILISHA MAISHA YA WATU MBEYA DC


Mwenyekiti wa Vituo vya taarifa na Maarifa wilaya ya Mbeya, Florah Mathias Mlowezi
Mwenyekiti wa Vituo vya taarifa na Maarifa wilaya ya Mbeya, Florah Mathias Mlowezi

Na Deogratius Temba

Ujenzi wa Harakati za  ukombozi wa wanawake Kimapinduzi katika ngazi ya jamii umesababisha mabadiliko makubwa ya kisera na kimfumo katika Halmashauri ya wilaya ya Mbeya.

Harakati zilizoanzishwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) mwaka 2011 kwa kufanya uraghibishi na kuanzishwa kwa vituo vya taarifa na Maarifa, uliwezesha watendaji wa serikali (halmashauri) kuelewa dhana ya usawa wa kijinsia na umuhimu wake katika kuwezesha wansichana kupata elimu sambamba na kuboresha miundombinu ya utoaji wa huduma za kijamii.

Akizungumza mwanaharakati, na mwenyekiti wa Vituo vya taarifa na Maarifa wilaya ya Mbeya, Florah Mathias Mlowezi, katika tamasha la Jinsia la 15 na Miaka 30 ya TGNP, kwenye Mdahalo wa Simulizi za mabadiliko, Changamto na Mikakati,  alisema TGNP ilipoingia katika halmashauri ya wilaya ya Mbeya imesababisha mabadiliko makubwa sana ambayo yamegusa maisha ya watu wengi masikini hasa watoto wa kike. 

“Wakati tunaanza Vituo vya Taarifa na Maarifa (KC) tulisomeaka vibaya sana, jamii ilituchukulia  tofauti kabisa, hawakuwa na uelewa juu ya sisi kwama tunalenga kufanya nini, tulionekana kama wapinzani au watu tunaotaka kuibua maovu tu. Mabadiliko ni mchakato, leo ukifika Mbeya utatusikia tumefanya mambo makubwa na sasa tunatambulika” alisema 

Ameongeza kwamba, suala la mimba na ndoa za utotoni lilikuwa ni tatizo kubwa kwa wilaya hiyo, hakuna aliyekuwa akitoa kipaumbele katika kulisimamia,  lakini uraghibishi uliofanywa na TGNP ulitusaidia uelewa mkubwa katika ngazi za chini kwenye kata na vijiji. 

Ameongeza kuwa wakati wa mrejesho wa uraghibish  kwa viongozi wa Halmashauri, kwasababu watu walikuwa hawajazoea kuona wananchi wa kawaida hasa wanawake wakizungumza waziwazi watu wengi walikuwa wanaamini kwamba, tatizo la mimba za utotoni ilisababishwa na wasichana kutaka kula viazi vya chips na vitu vitamu na kuelekeza lawama zote kwa waliopata ujauzito. 

Sasa hivi kwa kiasi kikubwa, uraghibish umeleta mabadiliko makubwa sana, baada ya shule maalum ya sekondari ya wasichana ya Gari jembe, kujengwa, na Halmashauri kudhamiria kujenga shule nyingine za wasichana kwa tarafa zingine ili kupunguza umbali kwa wasichana.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post