ASIYEJULIKANA ATUPA WATOTO MAPACHA PORINIHali ya taharuki imetokea katika eneo la Kihonda kwa Chambo Manispaa ya Morogoro mara baada ya wakazi wa maeneo hayo kukuta watoto mapacha wanaokadiriwa kuwa na umri wa siku moja wakiwa wametupwa porini huku miili yao ikiwa kwenye mfuko.

Tukio hilo limetokea leo Oktoba 13, 2023 Manispaa na Mkoa wa Morogoro na kuibua taharuki kwa wakazi wa eneo hilo.

Wakizungumza na vyombo vya habari mashuhuda wa tukio hilo wamelaani kitendo hicho cha watoto hao mapacha kutupwa porini  wakiwa wamepoteza maisha huku wakisema kuwa tukio hilo ni la mara ya kwanza kutokea katika eneo hilo.

Tayari miili ya watoto hao imechukuliwa na Jeshi la Polisi  kwa ajili ya uchunguzi zaidi ambapo Jeshi hilo limeahidi kutoa taarifa kwa vyombo vya habari mara baada ya uchunguzi kukamilika.

Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post