TANZANIA NA UZBEKISTAN KUSHIRIKIANA SEKTA YA UTALII

Na Mwandishi wetu. 

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Jasmine Kairuki (Mb),  amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Gavana wa jimbo la  Kharezm, jijini Samarkand - Uzbekistan, Bw. Davletov Anvar Kenjayevich, kuhusu ushirikiano katika sekta ya utalii baina ya Tanzania na Uzbekistan leo Oktoba 15, 2023.

Waziri Kairuki pia atapata nafasi ya kutembelea Chuo Kikuu cha Utalii ili kuona uzoefu wa Uzbekistan katika mafunzo ya sekta ya utalii; na kutafuta nafasi za  kujengewa uwezo kutoka kwao hasa ikizingatiwa kuwa jiji la Samarkand limeendelea kiutalii. 

Vilevile, Mhe. Kairuki na ujumbe wake wanatarajia kuona uzoefu ilionao Uzbekistan katika uratibu wa makumbusho za Taifa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post