WANAWAKE SHINYANGA WAMPONGEZA RAIS SAMIA KWA KULETA FEDHA ZA KUTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza kwenye kongamano la kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan

Na Amo Blog Shinyanga 

Wanawake  mkoani  Shinyanga  wamempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kupata PHD ya heshima huko Nchini India na kuleta Fedha nyingi za kutekeleza miradi mingi ya maendeleo katika sekta ya afya,elimu maji  na nishati ya umeme.

Kongamano hilo la kumpongeza Dkt. Samia limefanyika leo Oktoba ,12,2023 Manispaa ya Shinyanga likiongozwa na mkuu wa mkoa huo Christina Mndeme  na kuhudhuriwa na mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa Mabala Mlolwa na mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Simiyu  Shemsa Mohamed.

 Mndeme amewaeleza wanawake hao kuwa Serikali ya awamu ya sita imeleta Fedha nyingi za maendeleo na kila Kijiji kimefikiwa na mradi ambapo  sekta ya elimu  Serikali imeleta zaidi ya sh Bilioni 53.6 ikiwa  shule mpya 24 zimeongezeka,maabara 57 kwa shule za sekondari  na nyumba za walimu 69.

 Mndeme amesema  kwa upande wa nishati ya Umeme  Serikali  imeleta zaidi ya  sh Bilioni 323 kwa ajili ya mradi mkubwa wa  nishati ya Umeme jua unao tekelezwa kwenye Kijiji cha Talagha wilayani Kishapu ambao utakuwa ni mradi mkubwa  kwa Afrika Mashariki .

 "Umeme jua  utatarajia kutoa Megawati 150  na kuondokana na changamoto ya  wananchi kukosa Umeme kwa tatizo la  kukatikakatika",amesema Mndeme.

 Mndeme ameongeza kuwa katika sekta ya Afya  hospitali zilikuwa nane na sasa zimeongezeka  mbili na kufikia hospitali kumi  ambapo hospitali ya halmashauri Ushetu na  halmashauri ya wilaya ya Shinyanga zimeanza kufanya kazi  na Vituo vya afya vimeongezeka sita na kufikia 25 na Zahanati kumi na moja zimeongezeka na kufikia Zahanati 242.

 Serikali imeleta zaidi ya sh Bilioni  102  na kutekeleza miradi ya maji  47 sawa na ongezeko la miradi 15 huku miradi mipya 66 ikianzishwa  katika vijiji mbalimbali kwa lengo la kumtua ndoo mama kichwani.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akizungumza kwenye kongamano la kumpongeza Rais Samia Suluhu

Viongozi wanawake wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa akizungumza kwenye kongamano la kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan

Wanawake wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa akizungumza kwenye kongamano la kumpongeza Rais Samia Suluhu

Wanawake wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa akizungumza kwenye kongamano la kumpongeza Rais Samia Suluhu


Wanawake wakicheza kwenye kongamano la kumpongeza Rais Samia Suluhu
Wanawake wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa akizungumza kwenye kongamano la kumpongeza Rais Samia Suluhu






Wanawake wakicheza kwenye kongamano la kumpongeza Rais Samia Suluhu
Wanawake wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa akizungumza kwenye kongamano la kumpongeza Rais Samia Suluhu

Wanawake wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa akizungumza kwenye kongamano la kumpongeza Rais Samia Suluhu








Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post