Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imemteua Paul Makonda kuwa Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM akichukua nafasi ya Sophia Mjema aliyeteuliwa kuwa Mshauri wa Rais Masuala ya Wanawake na Makundi Maalum.
Makonda amewahi kushika nafasi mbalimbali ikiwamo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.