AZZA HILAL ATAMBULISHA RASMI KIWANDA CHA VIFUNGASHIO ‘AZAT’

Mkurugenzi wa Kiwanda Kidogo cha Kutengeneza Vifungashio cha AZAT ,Mhe. Azza Hilal Hamad akionesha vifungashio vinavyotengenezwa kwenye kiwanda cha AZAT kilichopo Nhelegani katika Manispaa ya Shinyanga.

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Mkurugenzi wa Kiwanda Kidogo cha Kutengeneza Vifungashio Rafiki kwa Mazingira 'AZAT' Mhe. Azza Hilal Hamad ametambulisha rasmi kiwanda hicho pamoja na vifungashio vinavyotengenezwa kwenye kiwanda hicho kilichopo Nhelegani katika Manispaa ya Shinyanga mkoani Shinyanga.

Mhe. Azza ametambulisha Kiwanda cha AZAT na bidhaa hizo leo Jumatano Oktoba 18,2023 wakati akisherehekea Siku yake ya kuzaliwa ‘Birthday’.

Mhe. Azza ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wadau kununua vifungashio hivyo ambavyo tayari vipo sokoni ili kukabiliana na changamoto ya uhaba wa vifungashio pamoja na kutunza mazingira.

“Katika kiwanda hiki cha AZAT tunatengeneza vifunganishio rafiki kwa mazingira kwa kutumia karatasi ngumu na bora. Kwa sasa tuna vifungashio aina tano na tunatengeneza kulingana na mahitaji ya mteja ,kuanzia robo kilo hadi kilo tano. Vifungashio hivi havilowani haraka. Hata ukihitaji nembo ya Biashara yako tuiweke, tunakuwekea kwenye vifungashio”,ameeleza Azza.

“Tunawakaribisha sana wadau wetu wakiwemo wafanyabiashara , wajasiriamali na wananchi wote. Vifungashio hivi ni bora na vigumu, vinafaa  kutumika kufungia bidhaa kwenye maduka ya dawa za binadamu, dawa za mifugo, Super Market, wauza chips, mama lishe, wauza matunda, Hotelini n.k”,ameongeza.

Amesema kwa yeyote anayehitaji vifungashio vya AZAT bidhaa tayari zipo kwenye maeneo mbalimbali au afike kwenye kiwanda cha AZAT kilichopo Nhelegani Mjini Shinyanga au apige simu namba 0787653394
Mkurugenzi wa Kiwanda Kidogo cha Kutengeneza Vifungashio cha AZAT ,Mhe. Azza Hilal Hamad akizungumza wakati akitambulisha Vifungashio vinavyotengenezwa kwenye kiwanda cha AZAT kilichopo Nhelegani katika Manispaa ya Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkurugenzi wa Kiwanda Kidogo cha Kutengeneza Vifungashio cha AZAT ,Mhe. Azza Hilal Hamad akizungumza wakati akitambulisha Vifungashio vinavyotengenezwa kwenye kiwanda cha AZAT kilichopo Nhelegani katika Manispaa ya Shinyanga.
Mkurugenzi wa Kiwanda Kidogo cha Kutengeneza Vifungashio cha AZAT ,Mhe. Azza Hilal Hamad akizungumza wakati akitambulisha Vifungashio vinavyotengenezwa kwenye kiwanda cha AZAT kilichopo Nhelegani katika Manispaa ya Shinyanga.
Mkurugenzi wa Kiwanda Kidogo cha Kutengeneza Vifungashio cha AZAT ,Mhe. Azza Hilal Hamad akionesha vifungashio vinavyotengenezwa kwenye kiwanda cha AZAT kilichopo Nhelegani katika Manispaa ya Shinyanga.
Mkurugenzi wa Kiwanda Kidogo cha Kutengeneza Vifungashio cha AZAT ,Mhe. Azza Hilal Hamad akionesha vifungashio vinavyotengenezwa kwenye kiwanda cha AZAT kilichopo Nhelegani katika Manispaa ya Shinyanga.
Mkurugenzi wa Kiwanda Kidogo cha Kutengeneza Vifungashio cha AZAT ,Mhe. Azza Hilal Hamad akionesha vifungashio vinavyotengenezwa kwenye kiwanda cha AZAT kilichopo Nhelegani katika Manispaa ya Shinyanga.
Mkurugenzi wa Kiwanda Kidogo cha Kutengeneza Vifungashio cha AZAT ,Mhe. Azza Hilal Hamad akionesha vifungashio vinavyotengenezwa kwenye kiwanda cha AZAT kilichopo Nhelegani katika Manispaa ya Shinyanga.
Muonekano wa sehemu ya vifungashio vinavyotengenezwa kwenye kiwanda cha AZAT kilichopo Nhelegani katika Manispaa ya Shinyanga.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post