ASKOFU MAGWESELA AWAPONGEZA WALIOFANIKISHA KUREJESHWA KWA SHULE YA BISHOP NKOLA

Askofu Mkuu wa Kanisa la Africa Inland Church Tanzania(AICT), Askofu Musa Magwesela akiwapongeza waumini wa kanisa la AICT Tanzania.

Na Amo Blog Shinyanga.

Askofu Mkuu wa Kanisa la Africa Inland Church Tanzania(AICT), Askofu Musa Magwesela amewapongeza waumini wa kanisa hilo kwa kutoa michango yao kiasi cha shilingi milioni 400 iliyofanikisha kurejesha Shule ya sekondari ya Bishop Nkola iliyopo katika Dayosisi ya Shinyanga

Askofu Magwesela amesema hayo leo Oktoba 26,2023 wakati akifungua kikao cha Baraza la Utendaji la Sinodi Kuu ya AICT Dayosisi ya Shinyanga kikao kilichofanyika kwa lengo la kujadili changamoto na mafanikio ya dayosisi hiyo.

Askofu Magwesela amesema jitihada zilizo fanywa na waumini wa kanisa la Africa Inland Church Tanzania (AICT) zinapaswa kupongezwa maana jitihada hizo zilifanikisha kurejeshwa kwa Shule ya Sekondari ya Askofu Nkola (Bishop Nkola Secondary School) iliyokuwa imeuzwa na hivyo kuleta aibu kubwa kwa kanisa.

Askofu Magwesela ameeleza kuwa shule hiyo ya kanisa iliuzwa kwa njia ya Mnada mnamo Februari 23, 2017 baada ya Dayosisi ya Shinyanga kushindwa kurejesha CRDB mkopo wa kiasi cha TZS 400,000,000.00 (Milioni Mia Nne) ambao shule hiyo iliwekwa kama dhamana.

Aidha Askofu Magwesela licha ya kuwapongeza waumini wa kanisa la AICT Tanzania pia amewaomba waumini kujitoa kuchangia ujenzi wa nyumba ya Askofu ambayo ujenzi wake umesimama kwa sasa kutokana na kukosekana kwa fedha ya kuendeleza ujenzi huo.

Naye katibu wa Kanisa la Africa Inland Church Tanzania(AICT) Mchungaji Josephales Mtebe ameeleza kuwa ili kudhibiti upotevu wa fedha na mali za kanisa wameajili wakaguzi wa takao fanya ukaguzi katika dayosisi zote za Kanisa hilo ili kubaini wabadhilifu wa fedha na mali za kanisa ndani ya kanisa la AICT.

Kwa upande wake Askofu wa kanisa la Africa Inland Church Tanzania(AICT) Dayosisi ya Shinyanga Askofu Zakayo Bugota amewaomba wajumbe wasinodi kuendelea kuhamasisha maendeleo ya Dayosisi hyo hali itakayo saidia kutimiza malengo na mipango waliyojiwekea katika kuchochea maendelea ya kanisa la Africa Inland Church Tanzania(AICT)

Hata hivyo Askofu Bugota amewasii wajumbe wasinodi kuendelea kuhamasisha michango kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya askofu ili ofisi hiyo iweke kukamilika kwa mda walio jiwekea na kuanza kufanya kazi.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Africa Inland Church Tanzania(AICT), Askofu Musa Magwesela akiwapongeza waumini wakanisa la AICT Tanzania kwa kujitoa kuchangia Maendeleo ya kanisa.
Askofu wa kanisa la Africa Inland Church Tanzania(AICT) Dayosisi ya Shinyanga Askofu Zakayo Bugota akimkaribisha kwa maombi askofu mkuu kwa ajili ya ufunguzi wa kikao cha sinodi.
Askofu wa kanisa la Africa Inland Church Tanzania(AICT) Dayosisi ya Shinyanga Askofu Zakayo Bugota akimkaribisha kwa maombi askofu mkuu kwa ajili ya ufunguzi wa kikao cha sinodi.
Katibu wa Kanisa la Africa Inland Church Tanzania(AICT) Mchungaji Josephales Mtebe akizungumza na wajumbe wa sinodi .
Piter Kamanda mkurugenzi wa kurugenzi ya mipango ,uwekezaji ,uchumi na maendeleo ya kanisa .
Katibu wa Kanisa la Africa Inland Church Tanzania(AICT) Mchungaji Josephales Mtebe akizungumza na wajumbe wa sinodi .
Askofu Mkuu wa Kanisa la Africa Inland Church Tanzania(AICT), Askofu Musa Magwesela akiwapongeza waumini wakanisa la AICT Tanzania kwa kujitoa kuchangia Maendeleo ya kanisa .
Askofu wa kanisa la Africa Inland Church Tanzania(AICT) Dayosisi ya Shinyanga Askofu Zakayo Bugota akimkaribisha kwa maombi askofu mkuu kwa ajili ya ufunguzi wa kikao cha sinodi.
Askofu wa kanisa la Africa Inland Church Tanzania(AICT) Dayosisi ya Shinyanga Askofu Zakayo Bugota akiteta jambo na katibu msaidizi wa Dayosisi ya Shinyanga Nuhu Manoni
Askofu wa kanisa la Africa Inland Church Tanzania(AICT) Dayosisi ya Shinyanga Askofu Zakayo Bugota akiteta jambo na katibu msaidizi wa Dayosisi ya Shinyanga Nuhu Manoni

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments