ALIYEJIHAMI KWA SILAHA YA HATARI AUA WATU 16


Takriban watu 16 wanahofiwa kuuawa katika shambulio la risasi katika mji wa Lewiston mjini Maine nchini Marekani.


Walisema kuwa anapaswa kuchukuliwa kuwa "mwenye silaha na hatari" na amewaambia wakazi wa Lewiston na Lisbon ya karibu wajihifadhi.

Polisi wamemtaja Robert Card, mwenye umri wa miaka 40, kama mshukiwa mkuu, wakisema kuwa "ana silaha ya hatari".

Mtu huyo mwenye silaha bado yuko huru mamia ya maafisa katika jimbo hilo wanahusika katika msako huo.

Mama mmoja ambaye alikuwa na familia yake wakati wa shambulio hilo, anasema alimlaza binti yake, 11, ili kumlinda.

Lewiston, mji mdogo wa karibu 38,000, umewekwa kwenye karantini huku biashara zimeambiwa kufungwa na watu kukaa nyumbani.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post