Tanzia : MWENYEKITI WA CCM MKOA WA ARUSHA ZELOTE STEPHEN AFARIKI DUNIA

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha, Zelote Stephen amefariki dunia jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.

Katibu wa CCM mkoa Arusha, Mussa Matoroka amesema wamepata taarifa za kifo hicho leo jioni Alhamis Oktoba 26,2023.

"Ni kweli Mwenyekiti amefariki jijini Dar es Salaam ambapo alikuwa amekwenda kupatiwa matibabu...huu ni msiba mkubwa kwetu CCM, familia ndugu na jamii," amesema Matoroka.

Katika ukurasa wake wa Instagram, Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo ameweka picha ya Marehemu Stephen huku akiandika maneno yanayoonyesha kuumizwa na kifo hicho.

Taarifa za kuondokewa na Zelote Stephen, Mwenyekiti wetu wa CCM mkoa wa Arusha ni taarifa za kusikitisha sana. Kwani kwa hakika kifo chake kimetunyima fursa muhimu ya kuendelea kujifunza mengi na kuuishi uongozi wake"

Mungu ameendelea kutufunza. Mipango yetu imekwama. Nenda Laigwanan. Nenda mzee wangu. Nilipokutembelea siku chache zilizopita hospitali ulinipa matumaini. Kumbe mipango ya Mungu ikabaki. Wewe ni shujaa, Nenda Kamanda", imesomeka sehemu ya taarifa hiyo.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments