TBS YASHIRIKI MAONESHO YA 20 YA WAHANDISI


Shirika la Viwango Tanzania (TBS ) limeshiriki katika maonesho ya 20 ya Wahandisi Jijini Dar es salaam, katika maonesho haya Shirika limepata nafasi ya kutoa elimu kwa wajasiriamali,wazalishaji wa bidhaa na Wahandisi.
Akizungumza katika maonesho haya Afisa Masoko TBS, Bi. Rhoda Mayungu ametoa wito kwa wahandisi kushiriki katika mchakato wa uandaaji wa viwango katika sekta mbalimbali kwa kutoa maoni na mapendekezo pale kiwango kinapowasilishwa kwa umma ili kupata maoni kabla ya kuhitimishwa, kwani wahandisi ni wadau muhimu.

"Shirika linapoandaa Viwango kabla ya kuhitimishwa hupelekwa kwa umma ili kupata maoni na mapendekezo endapo wahandisi watashirki kikamilifu katika hatua hii itasaidia wananchi kwani wao ni wadau muhimu sana” Alisema

Mmoja wa Wahandisi kutoka shirika hilo Bi. Christina John,amesema"Tupo hapa kwa ajili ya kuwaasa Wahandisi wenzetu ambao wana miradi ya kihandisi, Wahandisi wa majengo, mitambo,kemikali na wengine wote kwa ujumla wanapokua wanafanya miradi wahakikishe vifaa wanavyo tumia vimehakikiwa kwa ubora kwa ajili ya ubora wa miradi hiyo"Alisema

"Tunawaomba Wahandisi wanapotumia vifaa kwenye miradi yao wahakikishe wanatumia vifaa vilivyo thibitishwa na TBS,amewaomba wale ambao hawatumii vifaa vilivyothibitishwa,kulingana na sheria za Viwango wale wanao kiuka taratibu za ubora sheria zitatumika".Alisema


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post