MWONGOZO SHULE NYUMBANI WAZINDULIWA JIJINI DODOMA
WIZARA ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda, akinyanyua Miongozo mara baada ya kuzindua miongozo minne ya elimu maalum na jumuishi hafla iliyofanyika leo Septemba 12,2023 jijini Dodoma.

Na Alex Sonna-DODOMA

WIZARA ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda, amezindua miongozo minne ya elimu maalum na jumuishi ambayo inalenga kuboresha utoaji wa elimu kwa watoto wenye mahitaji maalum ikiwamo kuwafuata majumbani.

Miongozo hiyo ni pamoja na mwongozo wa shule ya nyumbani, ziara ya nyumbani, upimaji na ubainishaji na uendeshaji wa elimu maalum na jumuishi.

Akizindua miongozo hiyo leo Septemba 12, 2023 jijini Dodoma, Prof.Mkenda amesema miongozo hiyo italeta mabadiliko chanya miongoni mwa wadau katika kutimiza azma ya serikali ya kuwapatia fursa ya elimu bora wanafunzi wenye mahitaji maalum nchini.

Ametoa wito kwa viongozi, wakuu wa taasisi na wadau wanaojishughulisha na utoaji elimu maalum na jumuishi kuendelea kushirikiana na serikali kuhamasisha umuhimu wa elimu kwa watoto wenye mahitaji maalum.

“Natoa rai kwa familia na wadau wa maendeleo waendelee kuona umuhimu wa kuchangia juhudi za serikali katika kuwapatia huduma stahiki wanafunzi wenye mahitaji maalum ili kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika mchakato mzima wa ujifunzaji,”amesema.

Amehimiza wazazi kuona umuhimu wa kuandikisha watoto wote wenye mahitaji maalum katika shule kwa kuzingatia mahitaji ya mtoto.

“Kwa wale watakaohitaji huduma hii ipelekwe majumbani basi wawasiliane na sisi ili kuangalia namna tutakavyoweza kufikisha huduma hii nyumbani kwa mtoto,”amesema.

Aidha, amesema katika Rasimu ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 toleo la 2023 somo la elimu jumuishi na lugha ya alama litakuwa ni lazima kwa mtu yeyote anayeandaliwa kuwa mwalimu hapa nchini.

“Jitihada hizi kubwa mnazoziona zinatokana na msimamo wa Rais wetu Dkt.Samia Suluhu Hassan na nyie wote mnajua ni mashahidi maandalizi haya yalianza mapema na kama mnavyofahamu Rais wetu anataka kuhakikisha kila mtoto anakwenda shule,”amesema.

Ameishukuru Mfuko wa Serikali ya watu wa Uingereza (UKAID) kupitia program ya Shule Bora na Ali Kimara Foundation kwa kuchangia uandaaji na uchapishaji wa miongozo hiyo.Naye Mkurugenzi wa Elimu kutoka Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Susan Nussu, amesema katika sensa waliyoifanya ya watoto wenye mahitaji maalum hadi Machi mwaka jana walikuwa 66,000 na zaidi ya 55,000 wapo shule za msingi na wengine waliobaki wapo sekondari.

Awali, Mkurugenzi wa Elimu maalum wa Wizara hiyo, Dkt.Magreth Matonya amefafanua kuwa mwongozo wa shule ya nyumbani utasaidia kuhakikisha haachi nyuma mtoto yeyote kwenye upataji elimu.

Amesema mwongozo wa ziara ya nyumbani unakwenda kuwasaidia walimu wanaokwenda ziara za nyumbani kupata taarifa zitakazowezesha kuchukua hatua stahiki.

“Huu mwongozo wa shule ya nyumbani tumekuwa tukiusubiri sana tumekuwa na changamoto kwamba tuna watoto wengine hawawezi kukaa darasani kwa ajili ya changamoto za afya na ulemavu wa kiwango cha juu wao majumbani, tukaa tukasema tuanzishe ambao utasaidia kuhakikisha kwamba hatuwaachi nyuma kwenye upataji elimu,”amesema Dkt.MatonyaKadhalika, Mzazi wa Ali Kimara ambaye mtoto mwenye ugonjwa adimu, Sharifa Mbarak, ameshukuru serikali kwa kuzindua miongozo hiyo na kwamba ni hatua kubwa zilizopigwa na taifa katika utoaji elimu stahiki kwa kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum.WIZARA ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda, akizungumza wakati wa uzinduzi wa miongozo minne ya elimu maalum na jumuishi hafla iliyofanyika leo Septemba 12,2023 jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Elimu maalum wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt.Magreth Matonya,akitoa utangulizi kuhusu Miongozo wakati wa uzinduzi wa miongozo minne ya elimu maalum na jumuishi hafla iliyofanyika leo Septemba 12,2023 jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Elimu kutoka Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Susan Nussu,akizungumza wakati wa uzinduzi wa miongozo minne ya elimu maalum na jumuishi hafla iliyofanyika leo Septemba 12,2023 jijini Dodoma.

Kamishna wa Elimu Dkt. Lyabwene Mtahabwa,akizungumza wakati wa uzinduzi wa miongozo minne ya elimu maalum na jumuishi hafla iliyofanyika leo Septemba 12,2023 jijini Dodoma.

Mzazi wa Ali Kimara ambaye mtoto mwenye ugonjwa adimu, Sharifa Mbarak, akishukuru Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia kwa kuzindua miongozo minne ya elimu maalum na jumuishi hafla iliyofanyika leo Septemba 12,2023 jijini Dodoma.

Diwani wa Kata ya Makulu Hosea Shibago,akizungumza wakati wa uzinduzi wa miongozo minne ya elimu maalum na jumuishi hafla iliyofanyika leo Septemba 12,2023 jijini Dodoma.

SEHEMU ya Washiriki wakifatilia hotuba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda, (hayupo pichani) akizungumza wakati wa uzinduzi wa miongozo minne ya elimu maalum na jumuishi hafla iliyofanyika leo Septemba 12,2023 jijini Dodoma.WIZARA ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda, akipokea Tuzo iliyotolewa na Taasisi ya Ali Kimara Foundation kwa kutambua Mchango wake katika kuhimiza Elimu kwa Watoto wenye Magonjwa Adimu wakati wa uzinduzi wa miongozo minne ya elimu maalum na jumuishi hafla iliyofanyika leo Septemba 12,2023 jijini Dodoma.

WIZARA ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda,akizungumza mara baada ya kupokea Tuzo iliyotolewa na Taasisi ya Ali Kimara Foundation wakati wa uzinduzi wa miongozo minne ya elimu maalum na jumuishi hafla iliyofanyika leo Septemba 12,2023 jijini Dodoma.

WIZARA ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda,akikata utepe kuashiria uiznduzi wa miongozo minne ya elimu maalum na jumuishi hafla iliyofanyika leo Septemba 12,2023 jijini Dodoma.

WIZARA ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda, akinyanyua Miongozo mara baada ya kuzindua miongozo minne ya elimu maalum na jumuishi hafla iliyofanyika leo Septemba 12,2023 jijini Dodoma.WIZARA ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda, akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzindua miongozo minne ya elimu maalum na jumuishi hafla iliyofanyika leo Septemba 12,2023 jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna-DODOMA

WIZARA ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda, amezindua miongozo minne ya elimu maalum na jumuishi ambayo inalenga kuboresha utoaji wa elimu kwa watoto wenye mahitaji maalum ikiwamo kuwafuata majumbani.

Miongozo hiyo ni pamoja na mwongozo wa shule ya nyumbani, ziara ya nyumbani, upimaji na ubainishaji na uendeshaji wa elimu maalum na jumuishi.

Akizindua miongozo hiyo leo Septemba 12, 2023 jijini Dodoma, Prof.Mkenda amesema miongozo hiyo italeta mabadiliko chanya miongoni mwa wadau katika kutimiza azma ya serikali ya kuwapatia fursa ya elimu bora wanafunzi wenye mahitaji maalum nchini.

Ametoa wito kwa viongozi, wakuu wa taasisi na wadau wanaojishughulisha na utoaji elimu maalum na jumuishi kuendelea kushirikiana na serikali kuhamasisha umuhimu wa elimu kwa watoto wenye mahitaji maalum.

“Natoa rai kwa familia na wadau wa maendeleo waendelee kuona umuhimu wa kuchangia juhudi za serikali katika kuwapatia huduma stahiki wanafunzi wenye mahitaji maalum ili kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika mchakato mzima wa ujifunzaji,”amesema.

Amehimiza wazazi kuona umuhimu wa kuandikisha watoto wote wenye mahitaji maalum katika shule kwa kuzingatia mahitaji ya mtoto.

“Kwa wale watakaohitaji huduma hii ipelekwe majumbani basi wawasiliane na sisi ili kuangalia namna tutakavyoweza kufikisha huduma hii nyumbani kwa mtoto,”amesema.

Aidha, amesema katika Rasimu ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 toleo la 2023 somo la elimu jumuishi na lugha ya alama litakuwa ni lazima kwa mtu yeyote anayeandaliwa kuwa mwalimu hapa nchini.

“Jitihada hizi kubwa mnazoziona zinatokana na msimamo wa Rais wetu Dkt.Samia Suluhu Hassan na nyie wote mnajua ni mashahidi maandalizi haya yalianza mapema na kama mnavyofahamu Rais wetu anataka kuhakikisha kila mtoto anakwenda shule,”amesema.

Ameishukuru Mfuko wa Serikali ya watu wa Uingereza (UKAID) kupitia program ya Shule Bora na Ali Kimara Foundation kwa kuchangia uandaaji na uchapishaji wa miongozo hiyo.

Naye Mkurugenzi wa Elimu kutoka Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Susan Nussu, amesema katika sensa waliyoifanya ya watoto wenye mahitaji maalum hadi Machi mwaka jana walikuwa 66,000 na zaidi ya 55,000 wapo shule za msingi na wengine waliobaki wapo sekondari.

Awali, Mkurugenzi wa Elimu maalum wa Wizara hiyo, Dkt.Magreth Matonya amefafanua kuwa mwongozo wa shule ya nyumbani utasaidia kuhakikisha haachi nyuma mtoto yeyote kwenye upataji elimu.

Amesema mwongozo wa ziara ya nyumbani unakwenda kuwasaidia walimu wanaokwenda ziara za nyumbani kupata taarifa zitakazowezesha kuchukua hatua stahiki.

“Huu mwongozo wa shule ya nyumbani tumekuwa tukiusubiri sana tumekuwa na changamoto kwamba tuna watoto wengine hawawezi kukaa darasani kwa ajili ya changamoto za afya na ulemavu wa kiwango cha juu wao majumbani, tukaa tukasema tuanzishe ambao utasaidia kuhakikisha kwamba hatuwaachi nyuma kwenye upataji elimu,”amesema Dkt.Matonya

Kadhalika, Mzazi wa Ali Kimara ambaye mtoto mwenye ugonjwa adimu, Sharifa Mbarak, ameshukuru serikali kwa kuzindua miongozo hiyo na kwamba ni hatua kubwa zilizopigwa na taifa katika utoaji elimu stahiki kwa kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post