DEREVA BODABODA AFARIKI KWA KUGONGANA NA MWENDOKASI, RC CHALAMILA AKEMEA

Mtu mmoja aliyekuwa akiendesha pikipiki amefariki dunia katika ajali kati ya pikipiki hiyo na Gari ya Mwendokasi baada ya kugonga basi hilo kwenye eneo la Lumumba,  mataa ya Kituo cha Mwendokasi cha Fire na DIT Jijini Dar es Salaam.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limethibitisha kifo cha dereva huyo aliyedaiwa kuingia katika barabara ya mabasi ya mwendokasi na kuwa watatoa taarifa kamili ya tukio hili hapo baadaye.

Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amefika katika eneo hilo na kukemea vikali watu wote kupita kwenye barabara za mwendokasi bila vibali huku akibainisha kujana na mpango mahususi kwa bodaboda zinazokatisha kwenye mwendokasi na kusababisha ajali mara kwa mara.Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post