EMEDO YATOA MAFUNZO KWA WANACHAMA WA TMFD KUHUSU MRADI WA KUZAMA MAJI KWA WAVUVI

Na Tonny Alphonce,Dodoma

Waandishi wa habari za Uvuvi na Wanachama wa Taasisi ya waandishi wa habari ya kuendeleza shughuli za Bahari na Uvuvi(TMFD) wamepatiwa mafunzo ya siku moja na shirika la Usimamizi wa Mazingira na Maendeleo juu mradi wa kuzuia kuzama majini katika ziwa Victoria.

Waandishi hao waliopatiwa mafunzo hayo wametoka katika mikoa ya Mwanza, Dar es Salaam,Geita,Kagera na Pwani ambapo pia wamejulishwa juu ya mtandao wa kimataifa wa kuzuia kuzama maji Tanzania.

Akizungumza katika warsha hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa TMFD Edwin Soko amewapongeza waandishi hao wa habari kwa kuanza kubobea kwenye uandishi wa habari za aina moja ambao utasaidia habari nyingi kuandikwa kwa kina.
Mkurugenzi Mtendaji wa TMFD Edwin Soko akiongea na Waandishi wa habari za kuendeleza shughuli za Bahari na Wavuvi hawapo pichani.


Soko amesema ili waandishi waweze kuhamasika zaidi TMFD imeanza mchakato wa kuhakikisha habari Uvuvi zianze kushindanishwa na washindi waweze kupatiwa zawadi.

Akizungumzia mradi wa kuzuia kuzama maji unaotekelezwa na EMEDO, Soko amesema kwa waandishi wa habari za uvuvi kushiriki katika kuufahamu mradi huo ili waweze kuujulisha Umma hasa wavuvi juu ya umuhimu wa kuchukua tahadhari wanapokuwa majini.
Waandishi wa habari za kuendeleza shughuli za Bahari na Wavuvi wakiwa katika picha ya pamoja

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post