MKUU WA MKOA WA MANYARA APONGEZA UWEKEZAJI WA KIWANDA CHA MATI SUPER BRANDS LIMITED

 


Ferdinand Shayo ,Manyara .

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga amepongeza uwekezaji wa kiwanda cha kuzalisha vinywaji vikali cha Mati Super Brands Limited kilichopo Wilayani Babati Mkoani Manyara ambacho kimekuwa mstari wa mbele katika ulipaji kodi kwa serikali pamoja na kujitoa kusaidia jamii inayowazunguka kwa kutoa misaada mbalimbali.

Akizungumza mara baada ya kutembea kiwanda cha Mati Super Brands Limited,Mkuu wa Mkoa wa Manyara amepongeza kiwanda hicho kwa kuzalisha bidhaa zenye ubora pamoja na kutoa fursa za ajira kwa vijana wa Mkoa wa Manyara .


"Sisi kama serikali tunawapongeza kwa ulipaji mzuri wa kodi za serikali ambao unachangia Maendeleo kwa taifa lakini pia mmekuwa mstari wa mbele kujitolea katika masuala ya kijamii",amesema.

Sendiga amesema serikali itaendelea kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji ili waweze kufanya kazi zao bila usumbufu wowote.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kiwanda cha Mati Super Brands Limited David Mulokozi amepongeza serikali ya Awamu ya Sita ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira bora kwa wawekezaji na wafanyabiashara.

"Kwa sasa tuna serikali ambayo imeweka mazingira mazuri ya ulipaji kodi ambayo yanatoa fursa kwa wafanyabiashara kufanya kazi na kulipa kodi kwa hiari",ameeleza Mulokozi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post