VIJANA 27 WAPEWA SAKRAMENTI YA KIPAIMARA KANISA LA MT. ANDREA KITANGILI SHINYANGA... ASKOFU CHINYONG'OLE AWASIHI WAUMINI KULIOMBEA TAIFAAskofu Johnsoni Chinyong'ole wakanisa la Anglikana akiendesha Ibada katika Kanisa la Mtakatifu Andrea Kitandili Manispaa ya Shinyanga 

Na Mwandishi wetu Malunde Blog .

Askofu wa  kanisa la Anglikana Dayosisi ya Shinyanga Askofu Johnsoni Chinyong'ole ameongoza Ibada na kutoa sakramenti ya kipaimara kwa vijana 27 wanao sali katika kanisa la Mtakatifu Andrea Kitangili wakiume wakiwa 13 na wakike wakiwa 14 

Akitoa Sakramenti ya Kipaimara Askofu Chinyong'ole amempongeza mchungaji wa kanisa la Mtakatifu Andrea kwa kuwaandaa vijana hao katika misingi ya kumjua na mwenyezi mungu hali ambayo itasaidia kuongeza uwepo wavijana wenye uwezo wakulitangaza neno la Mungu.

Askofu Chinyong'ole amewasii waumini na viongozi wakanisahilo kuendelea kuliombea Taifa la Tanzania na viongozi wake katika kipindi hiki ambacho Taifa linatarajia kuingia katika uchaguzi wa serikali zamitaa mwaka 2024 ili waweze kuwachagua viongozi wenye kuwa na hofu ya Yungu.

Kwa upande wake mchungaji wa kanisa la Mtakatifu Andrea Kitangili Mchungaji Joan Ndabakubije (Mama Ndaba) amewashukuru viongozi wa dayosisi hiyo kwa kujitokeza kwa wingi katika ibada hiyo ya utoaji wa sakramenti ya kipaimara kwa vijana 27 wa kanisa hilo maana vijana hao watasaidia kuhamasisha vijana wengine wakujiunga katika kanisa hilo.

Mchungaji Joan Ndabakubije (Mama Ndaba) akimkaribisha Askofu wa  kanisa la Anglikana Dayosisi ya Shinyanga Askofu Johnsoni Chinyong'ole katika kanisa la Mtakatifu Andrea Kitangili.
Askofu wa  kanisa la Anglikana Dayosisi ya Shinyanga Askofu Johnsoni Chinyong'ole akiwa na mkewake katika kanisa la Mtakatifu Andrea Kitangili.

Vijana wakiwa na mchungaji wao katika picha ya pamoja baada ya kupewa sakramenti ya kipaimara.

Askofu wa  kanisa la Anglikana Dayosisi ya Shinyanga Askofu Johnsoni Chinyong'ole akiwa na mkewake pamoja na vijana walio pata sakramenti ya kipaimara.
Mchungaji Joan Ndabakubije (Mama Ndaba) akiwana viongozi wa kanisa la Mtakatifu Andrea  wakiandaa zawadi kwa ajili ya  kumkabidhi Askofu wa  kanisa la Anglikana Dayosisi ya Shinyanga Askofu Johnsoni Chinyong'ole .
Mchungaji Joan Ndabakubije (Mama Ndaba) akiwana viongozi wa kanisa la Mtakatifu Andrea  wakiandaa zawadi kwa ajili ya  kumkabidhi Askofu wa  kanisa la Anglikana Dayosisi ya Shinyanga Askofu Johnsoni Chinyong'ole .

Mchungaji Joan Ndabakubije (Mama Ndaba)  akiwa na vijana walio pewa kupewa sakramenti ya kipaimara.


Waumini wakimkabidhi Zawadi Baba Askofu.

Waumini wakimkabidhi Zawadi Baba Askofu.Waumini wakimkabidhi Zawadi Baba Askofu.

Waumini wakifatilia ibada katika kanisa la Mt.Andrea Kitangili.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post