KLINIKI YA ARDHI YAZINDULIWA TEMEKE






Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mhe. Mobhare Matinyi, akizungumza wakati wa uzinduzi wa kliniki ya ardhi siku ya Jumatano, tarehe 20/09/2023 katika viwanja vya Mbagala Zakhiem, wilayani humo, jijini Dar es Salaam.

*********

Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mhe. Mobhare Matinyi, tarehe 20 Septemba, 2023, alizindua zoezi la utoaji hati miliki za ardhi papo kwa papo kwa kutumia njia ya kielektronikia wilayani humo.

Uzinduzi huo ulifanyika katika viwanja vya Mbagala Zakhiem ambapo Mhe. Matinyi aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kupata huduma hiyo inayotoewa na Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi pamoja na Manispaa ya Temeke.

Zoezi hili la kurasimisha umiliki wa ardhi ni sehemu ya mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi unaofadhiliwa na Benki ya Dunia kwa kiasi shilingi bilioni 345.

Aidha, Mhe. Matinyi alisema kuwepo kwa mfumo huu wa urasimishaji umiliki wa ardhi kutasaidia wananchi katika masuala ya mirathi na uombaji mikopo katika taasisi za fedha.

Mhe. Matinyi pia alimshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutafuta fedha za mradi huu muhimu kwa maendeleo ya wananchi.

Naye Kamishna Msaidiziwa Ardhi Mkoa wa Dar es Salaam, Rehema Mwinuka, alisema serikali ina nia ya dhati ya kutatua kero za ardhi kwa wananchi kwa kuja na miradi mbalimbali ukiwemo huu wa uboreshaji usalama wa milki za ardhi.

"Wananchi ambao wana migogoro midogo midogo ambayo wameipeleka mahakamani na sehemu zingine wafike hapa ili wapatiwe utatuzi kwani mradi huo una hatua mbalimbali ikiwemo utoaji elimu na utoaji wa hati kwa vipande vilivyokamilika.

Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, Veronica Malangwa, alieleza kwamba zoezi la utoaji hati litapita katika mitaa mitano ya Manispaa ya Temeke na watatoa hati 3,244; hivyo kusaidia kupunguza kero za wananchi na kuboresha milki za ardhi.

Vile vile, Mwakilishi wa Benki ya Dunia, Aisha Masanja, aliipongeza serikali kwa kuwezesha kupatikana kwa miradi hiyo ambayo ni chachu ya maendeleo ya taifa na kwamba mradi huu umefadhiliwa kwa jumla ya shilingi bilioni 345 na utafanyika katika halmashauri zote za mkoa wa Dar es salaam na halmashauri 41 nchini kote.

Kaimu Mkurugenzi Manispaa ya Temeke Veronica Malangwa, akizungumza na wananchi waliojutokeza kwenye uzinduzi huo.


Mwakilishi kutoka world bank amabao ndiyo wafadhili wa mradi huo Aisha Masanja akiztoa salamu sake na pongezi kwa serikali kufanikisha mradi huo.



Kamisha wa ardhi mkoa wa Dar es Salaam Rehema Mwinuka akizungumzia juu ya mradio huo wa klinik ya ardhi.






Baadhi ya wakazi wa milaya ya Temeke wakipewa hati Miliki na Mkuu Wa Wilaya ya Tameke Mubale Matinyi mapema Leo Dar es salaaam.
Baadhi ya wakazi wa milaya ya Temeke wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu Wa Wilaya ya Tameke Mubale Matinyi mapema Leo Dar es salaaam.







Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post