MOBIKEY YASHAURI WAKULIMA KUTUMIA TEKNOLOJIA ZA KISASA

 


Na Dotto Kwilasa, Malunde1 Blog, DODOMA.


Maonesho ya wakulima Kanda ya kati yakiwa yanaendelea Jijini hapa, wakulima wameshauriwa kutumia nafasi hiyo kujifunza mbinu Bora za uzalishaji mazao kupitia teknolojia za kisasa.

Afisa Mauzo wa Kampuni ya Mobikey inayojihusisha na usambazaji wa bidhaa za Kilimo Snasha Ayubu ameeleza hayo leo Agosti 5,2023 Jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari na kueleza kuwa matumizi ya teknolojia za kisasa inaongeza mazao mara dufu.

Ayubu amesema huu ni ulimwengu wa Sayansi na Ubunifu hivyo wakulima wanapaswa kuachana na matumizi ya jembe la mkono na kujikita Katika zana za kisasa ikiwemo ikiwemo trekta.

Aidha ameeleza kuwa shughuli zinazofanywa na Kampuni hiyo kuwa ni pamoja na kuwaonesha njia wakulima kutumia bidhaa za Kilimo zenye ubora na za kisasa Ili kuendana na ulimwengu wa Sayansi.

"Ili kupata mazao mengi Lazima wakulima wakubali kubadilika na kuanza kutumia zana za Kilimo za kisasa, lakini Kwa kuzingatia uhifadhi wa mazingira Ili kuwa na Ardhi yenye rutuba Hali itakayosaidia mazao kuwa mengi,"amesema

Pamoja na hayo ametumia nafasi hiyo kutaja sehemu ambazo Mobikey inafanya kazi ya kuwauzia zana za Kilimo wakulima kuwa ni Dodoma,Katavi,Mbeya,Babati,Kahama na sehemu nyingine.

"Tunawauzia wakulima zana za kisasa ikiwemo powertela,matrekta,haro na nyingine,kwa wateja wanaonunua matrekta huwa tunawapa zawadi ,ofa hii pia huwa inawahusu watu pia wanaotuletea wateja,"amesema



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post