SPIKA WA BUNGE AZUIA MJADALA WA BANDARI BUNGENI


Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson amezuia mjadala wa mkataba wa bandari kujadiliwa ikiwa tayari Bunge limeshamaliza majukumu yake ya awali, huku akisema linaweza kujadiliwa endapo litaletwa katika utaratibu mwingine wa kibunge.


Spika Dk Tulia ametoa kauli hiyo leo Jumanne Agosti 29, 2023, muda mfupi baada ya kipindi cha maswali na majibu ya wabunge ambapo amesema kuwa Bunge lilishamaliza mjadala huo hivyo wabunge wanatakiwa kuendelea kuwasikiliza wananchi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post