WATU 35 WAREKEBISHWA SURA BUGANDO

Mfano mtu akifanyiwa upasuaji wa uso
**
Wagonjwa 35 wamefanyiwa upasuaji wa kurekebisha sura (plastic surgery) na madaktari bingwa kutoka nchini Marekani wakishirikiana na wenzao wa Hospitali ya Kanda Bugando (BMC) jijni Mwanza.


Akizungumzia upasuaji huo Daktari Bingwa wa Upasuaji Sanifu kutoka BMC, Francis Tegete amesema wagonjwa hao ni kati ya 55 waliofanyiwa vipimo.


Upasuaji huo uliofanyika Agosti 21 hadi 25 mwaka huu katika hospitali ya Bugado chini ya madaktari bingwa wa upasuaji sanifu wa uso, pua, koo, na masikio kwa kushirikiana na wataalamu, manesi na madaktari pia ulihusisha madaktari bingwa 22 kutoka Shirika la Healing the Children North East lililopo nchini Marekani.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post