Picha : SIMBA DAY UNYAMA MWINGI...RAIS SAMIA ASHUHUDIA POWER DYNAMO WAKILA KICHAPO CHA SIMBA SC


Shamra shamra za Washabiki na Wapenzi wa timu ya Simba kwenye Tamasha la Simba Day 2023 lilofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa, Temeke Jijini Dar es Salaam tarehe 06 Agosti, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Wachezaji wa timu ya Simba kabla ya kuanza kwa mchezo baina ya Simba na Power Dynamos ya Zambia uliofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa Temeke Jijini Dar es Salaam tarehe 06 Agosti, 2023.

Rais Dkt. Samia ameshuhudia mchezo huo ambapo Power Dynamo ya Zambia imefungwa magoli 2-0 na Simba SC kwenye. Mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliopigwa uwanja wa Taifa katika tamasha la Simba lililofabyika Leo Jumapili Agosti 6, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Wachezaji wa timu ya Simba kabla ya mechi na timu ya Power Dynamos ya Zambia iliyofanyika kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, Temeke Jijini Dar es Salaam tarehe 06 Agosti, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Wachezaji wa timu ya Power Dynamos ya Zambia kabla ya mchezo na Simba uliofanyika kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, Temeke Jijini Dar es Salaam tarehe 06 Agosti, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi ya Jezi ya Timu ya Simba kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba Salim Abdallah Try Again wakati wa Sherehe za Simba Day 2023 zilizofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa, Temeke Jijini Dar es Salaam tarehe 06 Agosti, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Jezi ya Simba mara baada ya kukabidhiwa kwenye Tamasha la Simba Day 2023 lililofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa Temeke Jijini Dar es Salaam tarehe 06 Agosti, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Tuzo ya Shukran kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba Salim Abdallah Try Again wakati wa Sherehe za Simba Day 2023 zilizofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa Temeke Jijini Dar es Salaam tarehe 06 Agosti, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia katika kilele cha Tamasha la Simba Day 2023 lililofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa, Temeke Jijini Dar es Salaam tarehe 06 Agosti, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa kwa ajili ya Tamasha la Simba Day 2023 Temeke Jijini Dar es Salaam tarehe 06 Agosti, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na Viongozi wengine wakati akiangalia mechi kati ya Simba na Power Dynamos ya Zambia iliyofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa, Temeke Jijini Dar es Salaam tarehe 06 Agosti, 2023.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post