ALIYEKUWA MKURUGENZI JIJI LA ARUSHA AFUNGWA JELA MIAKA 20

Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imewahukumu kifungo cha Miaka 20 aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, Dkt John Pima na wenzake wawili baada ya kukutwa na hatia kwenye makosa ya uhujumu uchumi.

Hukumu hiyo imetolewa Leo Agosti 31, 2023 Hakimu Seraphin Nsana wa Mahakama ya Hakimu mkazi Arusha baada ya kujiridhisha pasina Shaka juu ya ushahidi uliotolewa mahakamani hapo kwa pande zote mbili.

 Wengine Waliohukumiwa katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi, aliyekuwa Mweka Hazina wa jiji la Arusha, Mariam Mshana na aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji, Innocent Maduhu.

Hakimu Nsana amesema hukumu hiyo ameitoa kwa kuzingatia sheria, baada ya Maombi ya Mawakili ya Pande zote mbili, ikiwemo washtakiwa kutokuwa na rekodi ya makosa ya nyuma, kutegemewa na Familia, pamoja na ushirikiano walioutoa kwa kipindi chote cha mwenendo wa Kesi.

Kwa Kuzingatia hayo, akawahukumu kifungo jela cha Miaka 20, huku miezi kumi na minne waliyokuwa kizuizini ikizingatiwa

Hata hivyo dkt John Pima na Wenzake wana haki ya kukata rufaa endapo hawajaridhishwa na hukumu hiyo.

Dkt Pima na Wnzake walikuwa Wakikabiliwa na mashataka 9 ikiweno ya utakatishaji wa kiasi cha milioni 103.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post