TGNP WAFANYA ZIARA KWENYE MIRADI YA MAENDELEO NDANI NA NJE YA KISHAPU


Vituo vya taarifa na maarifa Wilayani Kishapu Mkoani Shinyangan vikiwa kwenye picha ya pamoja na kibao cha SIDO,Agosti 13,2023 wakiwa kwenye ziara na TGNP.

Na Halima Khoya,Kishapu

Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) umefanya ziara ya kutembelea miradi iliyo hai Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga mara baada ya kutoa mafunzo ya Ujasiriamali kwa vituo vya taarifa na maarifa Wilayani humo ili kujifunza mbinu na kuelewa namna ya kuendesha miradi mbali mbali.

Zoezi hilo limefanyika Agosti 13,2023 ambapo walitembelea miradi mbali mbali nje na ndani ya Wilaya hiyo na kubaini fursa na maendeleo makubwa ya kiuchumi yatokanayo na udhubutu wa baadhi ya wajasiriamali.

Akizungumza baada ya kutamatisha ziara hiyo,Frida Saidi amesema wanaishukuru (TGNP) kwa kuwapa mwangaza kwenye ujasiriamali wao kwa kuwakutanisha na wataalamu kutoka Shirika la kuhudumia viwanda vidogo (SIDO) na wajasiriamali wenye miradi.

“Tumeanza kujifunza kwa nadharia,vile vile tumepata nafasi ya kutembezwa kwenye miradi mbalimbali,tumepata ujuzi wa kuendesha miradi na biashara shughuli zetu,ytunaamini mwanamke akiwezeshwa anaweza,tunaishukuru sana TGNP kwa kutuwezesha kiujuzi wanawake”amesema Frida.

Nae mmiliki wa mradi wa kufuga kuku Wilaya ya Kishapu,Edina Kaluta amesema ameweza kuuendeleza mradi wake kwa kuthubutu baada ya kupatiwa mafunzi kutoka kwenye shirika la Grown women linaloshirikiana na TGNP 2021 lililokuwa likitoa elimu ya jinsia,haki na usawa na mwanamke na uongozi sambamba na kufanya kongamano la siku tano.

“Mwanamke anayetaka kujikita na ufugaji wa kuku,ninawakaribisha sana na nitatoa elimu niliyonayo kwa wenye uhitaji na uthubutu,TGNP imenisidia sana hadi kufikia hapa ninafuga kuku Zaidi ya 700 wa kisasa na wakienyeji” amesema Kaluta.
Vituo vya taarifa na maarifa Wilayani Kishapu Mkoani Shinyangan wakiendelea na ziara ya kutembelea miradi,wakiwa kwenye Shirika la kuhudumia viwanda vidogo Mkoani humo (SIDO) agosti 13,2023.
Vituo vya taarifa na maarifa Wilayani Kishapu Mkoani Shinyangan wakiendelea na ziara ya kutembelea miradi,wakiwa kwenye mradi wa kuku agosti 13,2023.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post