MASHABIKI WA SIMBA SC, YANGA SC WACHINJA NG'OMBE KUSHEREHEKEA SIMBA DAY KASHISHI - KAHAMA


Mashabiki wa Simba SC katika kata ya Kashishi, halmashauri ya Msalala wilaya ya Kahama wakiwa na ng'ombe waliyechinja siku ya Simba Day na kusherehekea kwa kula chakula cha pamoja kwa kuwaalika watani wao wa jadi wa timu ya Yanga SC pamoja na jamii. Picha na Patrick Mabula
Mbalimbali za matukio ya Mashabiki wa Simba wa kata ya Kashishi , halmashauri ya Msalala , wilayani Kahama walipochinja ng'ombe wawili na kula chakula cha pamoja na watani zao wa Yanga SC pamoja na jamii ya kata hiyo kwa lengo la kuimarisha upendo, mshikamano na umoja miongoni mwao 

Na Patrick Mabula , Kahama .

Mashabiki wa timu ya Simba katika kata ya Kashishi , halmashauri ya Msalala , wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga wamesherehekea Simba Day kwa kuchanga na fedha na kusaidia katika suala la elimu.


Mashabiki hao waliokuwa wameandaa chakula cha pamoja na kuwaalika watani wao wa Yanga SC na wanajamii wa kata ya Kashishi wachinja kitoweo cha ng’ombe wawili ambapo katika sherehe hiyo walichanga fedha ambazo watazikabidhi katika kusaidia suala la elimu.


Akiongea katika hafla hiyo mmoja wa viongozi wa tawi la Simba SC katika kata hiyo Manungu Mahumbi alisema waliamua kusherehekea Simba Day kwa kuandaa chakula cha pamoja na kuwaalika watani wao wa jadi wa timu ya Yanga  SC pamoja na jamii wanayoishi nayo.

Vumilia Nyerere alisema lengo la kuandaa chakula hicho na kula pamoja ni kuwa siku zote utani wa jadi katika michezo siyo uadui bali na kudumisha urafiki , upendo na mshikamano miongoni mwao.


“Chakula tulichoandaa katika kufurahia siku ya Simba day na kula pamoja na watani zetu wa jadi wa Yanga pamoja na jamii tunayoishi nayo ni kuendeleza urafiki, ndungu miongoni mwetu",alisema Nkuba Aljabili .

Nao mashabiki wa Yanga SC wakiongea katika hafla hiyo Jidasagula John na Philipo Jackson waliwashukuru watani zao wa Simba SC kwa mpango huo kwa sababu siku zote utani wa Simba na Yanga kupitia michezo siyo uadui bali ni kudumisha urafiki ,umoja na mshikamano.

Naye Sali Buzali alisema waliona katika kusherehekea Simba day wasiishie kula chakula pekee bali waliamua kuchanga fedha ambazo watazikabidhi katika moja ya shule ya msingi iliyopo kijiji cha Mwamboku ziweze kusaidia katika suala la kutatua sehemu ya changamoto zilizopo hapo zinazowakabili watoto wao.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post